Posts

KAFULILA AELEZEA MKAKATI WA KUVUTIA SHILINGI TRILIONI 21 ZA PPP

Image
Na Benny Mwaipaja, Arusha Serikali inapanga kukutanisha wakuu wa mashirika ya umma 7 ya kimkakati na wabobezi wa uwekezaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) mwezi ujao kwa lengo la kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuvutia mitaji ya kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 9 (sawa na Sh. trilioni 21) ndani ya miaka mitatu. Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila. alisema kuwa mkutano huo utakaofanyika Mei 2-6 ni sehemu ya mkakati wa kufikia malengo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDPIII). Alisema Mpango huo umeainisha mahitaji ya fedha zitakazotumika kuutekeleza kuwa shilingi trilioni 114 ambapo kati ya fedha hizo, zaidi ya shilingi trilioni 60 zinatakiwa kutoka Serikalini na kiasi kilichobaki cha sh. trilioni 40.3 kinatarajiwa kutoka Sekta Binafsi. “Katika mgawanyo huo, zaidi ya Shilingi trilioni 21, sawa na asilimia 17 ya ugharamiaji wa mpango huo, z...

SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI ZIRUDISHE MAZOEZI KWA WANAFUNZI

Image
  Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati akizindua Mkutano wa Kikundi cha Utafiti wa Magonjwa ya Kisukari na magonjwa Yasiyo ambukiza kwa ukanda wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam. @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ NA. WAF – Dar es Salaam Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka shule zote za msingi na sekondari nchini kuwepo na mazoezi ya viungo kwa wanafunzi ikiwepo kukimbia, mchakamchaka, kutembea na kucheza ngoma au mpira kwa lengo la kupunguza Magonjwa Yasiyo Ambukiza. Hayyo yamesemwa wakati akizindua Mkutano wa Kikundi cha Utafiti wa Magonjwa ya Kisukari na magonjwa Yasiyo ambukiza kwa ukanda wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam. “Nitoe wito kwa Watanzania mazoezi sio lazima uende ‘Gym’ wala sio lazima ukimbie lakini ukipata hata dakika angalau 30 kwa siku kwa kutembea na ukatoka jasho inatosha.” amesema Waziri Ummy Aidha, Waziri Ummy amesema lengo la kuzindua kikundi hicho ni kujadili kwa pamoja jinsi ya kuboresha huduma kwa watu wenye ugonjwa w...

WAZIRI MKUU AFUNGUA VITUO VYA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chamwino  jijini Dodoma, Aprili 26, 2023.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mborouk , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamai Masauni, Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John William Masunga, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Anamringi Macha na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati  ya Bunge  ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama,  Vita Kawawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chamwino n jijini Dodoma, Aprili 26, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya, mkuu wa Mkoa a Dodoma, Rosemary Senyamule, Kamshina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John William Mas...

UHOLANZI YARIDHISHWA NA MAZINGIRA YA BIASHARA, DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA

Image
Uholanzi imeoneshwa kuridhishwa na mazingira ya biashara na uwekezaji, demokrasia, haki za binadamu na utawala bora nchini. Hayo yamebainishwa na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Wiebe de Boer wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam. Balozi Boer alisema mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini wafanyabiashara wengi kutoka Uholanzi wamewekeza Tanzania. “Kadhalika tumefurahishwa na kuridhishwa na demokrasia nchini, haki za binadamu na utawala bora pamoja na kufunguliwa kwa majukwaa na mikutano ya kisiasa nchini,” Alisema Balozi Boer. Mbali na kuwekeza katika biashara na uwekezaji pia wafanyabiashara wa Uholanzi wamewekeza pia katika sekta za utalii pamoja na kilimo. Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alieleza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa karibu na ushirikiano uliopo kati ya pande zote mbili. Dkt. Tax al...

MOROGORO KUANDAA SHEREHE ZA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI KITAIFA MWAKA HUU-PROFESA ADALICHAKO

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya usalamam,Afya Mahali pa Kazi Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Osha jijini Dodoma leo. Siku ya  Usalama Pahala pa kazi Duniani ilianza Mwaka 1996 nchini Marekani katika Jiji la  New York nchini Marekani  ambapo waathirika wa watu walioumia na kupoteza maisha wakiwa kazini, hukumbukwa maadhimisho hayo yalikuwa yakifanywa  na Chama cha Wafanyakazi Duniani iliopofika mwaka 2001 Shirika la kazi Duniani liliona kuwa ni busara kunbadilisha madhumuni ya siku hiyo na kuita siku ya usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani, Waziri ndalichako aliendele kusema  kwa hapa Tanzania siku hiyo ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2004 tangu wakati huo imekuwa ikianzimishwa kila mwaka , ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika kwa mara ya 19. Maadhimisho hayo yamekuwa yakilatibiwa na serikali kupitia taasisi...

HONGERA MHANDISI ARON KWA KUMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KWA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA UMMA

Image
Kesho inatimia miaka 59  ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, leo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamure ,amezindua mradi wa ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia maji safi lenye ujazo wa lita Milioni 2.5 lililopo Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma. Uzinduzi huo ni moja ya sherehe za muungano mbazo zitafikia kilele chake kesho nchi nzima ambapo tofauti na miaka ya nyuma husherekewa mjini kwa magwalide sasa ni vijijini wilayani na kata na mikoa huku zikiwashirikisha wananchi ili wazidi kuuelewa muungano sawasawa. Mradi wa Tanki hilo umegharimu Shilingi Bilioni 1,6 badara ya Shilingi Bilioni 2.5 zilizokuwa zimetengwa kutumika hapo awali, kabla ya kumpata mkandalasi wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT na kuamua Duwasa kununua vifaa vya ujenzi na kumpatia mjenzi ndipo walipoweza kusevu nusu ya fedha iliyokadiliwa kutumika, Mkuu wa mkoa amewapongeza viongozi wa Duwasa, chini ya Mkurugemzi Mtendaji wake Mhandisi Aron Joseph. Mradi huo utaweza kuwezesha kuongeza upatikanaji wa maji...