MOROGORO KUANDAA SHEREHE ZA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI KITAIFA MWAKA HUU-PROFESA ADALICHAKO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya usalamam,Afya Mahali pa Kazi Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Osha jijini Dodoma leo. Siku ya Usalama Pahala pa kazi Duniani ilianza Mwaka 1996 nchini Marekani katika Jiji la New York nchini Marekani ambapo waathirika wa watu walioumia na kupoteza maisha wakiwa kazini, hukumbukwa maadhimisho hayo yalikuwa yakifanywa na Chama cha Wafanyakazi Duniani iliopofika mwaka 2001 Shirika la kazi Duniani liliona kuwa ni busara kunbadilisha madhumuni ya siku hiyo na kuita siku ya usalama na Afya Mahali pa kazi Duniani, Waziri ndalichako aliendele kusema kwa hapa Tanzania siku hiyo ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2004 tangu wakati huo imekuwa ikianzimishwa kila mwaka , ambapo mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika kwa mara ya 19. Maadhimisho hayo yamekuwa yakilatibiwa na serikali kupitia taasisi yake ya OSHA kwa kushirikiana na wadau wa utatu ambao ni Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA), Chama cha Waajili Tanzania (ATE), Pamoja na Shirika la kazi Duniani (ILO).
Kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanafanka kitaifa mkoani Morogoro lengu kubwa la kampeni hiyo ni kuendeleza kampeni ya kuhamasisha kuweka mazingira salama sehemu pa kazi ,miongoni mwa wadau kupitia kaulimbiu mbalimbali ambazo hutolewa na Shirika la kazi Duniani ,Kaulimbiu ya Mwaka huu ni Mazingira Salama na Afya kazini ni kanuni ya Afya msingi mahali pa kazi
Kaulimbiu hiyo inatokana na Azimio la Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), katika kikao cha Juni 2022 kilichofanyika Gineva Uswizi na kuamua swala la usalama na Afya mahali pa kazi liwe mojawapo ya kanuni na haki tano za msingi kwa Wafankazi mahali pa kazi. Kanuni na haki nyingine za Msingi kwa wafanyakazi ni uhuru wa kujumuika na haki ya majadiliano kazini . kukomesha aina zote za kazi za kulazimishwa. kukomesha ajira za watoto,a kuondolewa kwa ubaguzi katika swala la ajira na kazi.
Waziri Ndalichako alisema kwamba ,takwimu za Kidunia zilizotolewa na Shilaka la kazi Duniani (ILO) zinaonyesha zaidi ya mwaka 2022 watu milioni mbili na laki tisa (2.9) hupoteza maisha kutokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Pia zaidi ya wafanyakazi milioni 402 huumia wakiwa kazini na kusababisha kushindwa kutekeleza majukumu yao yakiwemo ya kifamilia na kuwa kwenye matibabu hadi wanapopona
Baadhi ya Maofisa wa OSHA wakiwa katika hafla hiyo
Rais wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) Nyamhokya akisikiliza kwa makini maswali ya wanahabari
Wanahabari wakimsikiliza Waziri
Waziri Ndalichako, akibadilishana mawazo na mwenyeji wake pamoja na Nyamhokya
Mwakilishi wa Chama cha Waajili nchini (ATE) akizungumza
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), akizungumza na wanahabari
Waziri akipiga picha na maofisa kutoka Taasisi zinazohusiana na wafanyakazi Duniani
Comments
Post a Comment