HONGERA MHANDISI ARON KWA KUMUUNGA MKONO RAIS DKT. SAMIA KWA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA UMMA

Kesho inatimia miaka 59  ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, leo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamure ,amezindua mradi wa ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia maji safi lenye ujazo wa lita Milioni 2.5 lililopo Kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

Uzinduzi huo ni moja ya sherehe za muungano mbazo zitafikia kilele chake kesho nchi nzima ambapo tofauti na miaka ya nyuma husherekewa mjini kwa magwalide sasa ni vijijini wilayani na kata na mikoa huku zikiwashirikisha wananchi ili wazidi kuuelewa muungano sawasawa.

Mradi wa Tanki hilo umegharimu Shilingi Bilioni 1,6 badara ya Shilingi Bilioni 2.5 zilizokuwa zimetengwa kutumika hapo awali, kabla ya kumpata mkandalasi wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT na kuamua Duwasa kununua vifaa vya ujenzi na kumpatia mjenzi ndipo walipoweza kusevu nusu ya fedha iliyokadiliwa kutumika, Mkuu wa mkoa amewapongeza viongozi wa Duwasa, chini ya Mkurugemzi Mtendaji wake Mhandisi Aron Joseph. Mradi huo utaweza kuwezesha kuongeza upatikanaji wa maji  kutoka asilimia 42 hadi asilimia 87 katika wilaya ya Chamwino."Nawapongeza Duwasa wote kwa ubunifu  huu kuokoa fedha nyingi za Serikali kwa kubuni namna nzuri ya usimamizi wa ununuzi wa vifaa na kumkabidhi Mkandarasi  Suma JKT  hayo ni matumizi mazuri", alisema Senyamure.Aidha Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wananchi wawe walinzi wazuri wa vyanzo vya maji.

Aidha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kamikimba amesema Kitaifa  upatikanaji wa maji  umefikia asilimia 37 na asilimia 88 wanapata maji mijini, aidha Katibu huyo alibainisha kwamba miradi inayotekelezwa kwa mkoa wa Dodoma ni uchimbaji wa Visima maeneo ya Pembezoni ambapo Bilioni 4,8 zitatumika eneo la Nzuguni kuchimba visima ambapo utazalisha maji lita milioni 7 kwa siku na unatarajiwa kukamilika mwezi wa nane mwaka huu. Katibu huyo alisema Miradi mikubwa wa maji kwa miji 28 Chamwino ikiwemo unaendelea na mkandarasi anaendelea na ukikamilika kutakuwa na uhakika wa kupunguza changamoto za maji . Naye Naibu Katibu Mkuu Muungano Abdallah  Hassan Mitawi alibainisha kwamba mwaka huu wamekuja tofauti katika kusherekea muungano na tofauti itasaidia kupeleka kwa wenye muungano ambao ni wananchi na ukiambatana na sherehe za uzinduzi wa miradi mbalimbali  nchini. Baadhi ya wakazi wa Chamwino waliozungumza katika hafla hiyo  walimpongeza Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan pamoja na Mhandisi wa Duwasa kwa kuweza kufanikisha upatikani wa maji ya uhakika wilayani kwao wameomba aendelee na moyo huo ili nchi isongembele kwa maendeleo

Senyamure akiwatunza wasanii wa wilaya ya Chamwino waliokuwa wakitoa Burudani katika hafla hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kamikimba, akizungumza katika hafla hiyo
Naibu Katibu Mkuu Muungano Abdallah Mitawi, akiwasili katika hafla hiyo

Mkurugenzi Mkuu wa DUWASA Mhandisi Aron (kulia), akiwa na viongozi katika uzinduzi wa mradi huo


Mkuu wa Mkoa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, wakisalimiana  baada ya kukutana


Mkurugenzi wa Duwasa, Mhandisi Aron, akisoma taarifa za ujenzi wa Tanki hilo kwa mkuu wa mkoa na Katibu Mkuu



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, akipokea risala toka kwa Mkurugenzi wa DUWASA Mhandisi  Aron Joseph
Mkuu wa mkoa akikata utepe kuzindua tanki hilo


Mkuu wa mkoa akimtwisha ndoo ya  maji baada ya kukingwa kutoka katika tanki hilo.
Mkurugenzi Mhanndisi Aron Joseph, akimuonyesha ujazo wa taifa


Wanahabari wakitoka katika uzinduzi huo


Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Nadhifa Kimkimba, akizungumza katika hafla hiyo



Naibu Katibu Mkuu Muungano, Mitawi, akitunza wasanii
Mkurugenzi Aron, akitunza wasanii
 

Wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi lasmi

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA