WAJUMBE TUGHE WAMLA KICHWA KATIBU MKUU WAO HERY MKUNDA , WAMPA SHAVU ALIYEKUWA NAIBU WAKE RUGEMALIRA

'

Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama Tughe ngazi ya Taifa uliofanyika leo wamemchagua Katibu Mkuu Mpya kwa ajili ya kukiongoza chama hicho kwa miaka mitano naye ni Rugemalira Rutatina (pichani anayepongezwa na wajumbe) ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho



Wajumbe hawa walionekana tangu mapema katika ukumbi wa mkutano wa Mabele jijini Dodoma kwamba wanataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa chama hicho wakiimba kwa hisia kali wimbo wa Mshakamano na wa Taifa, hata ilipofika kunyosha mikono kwa ajili ya kutaka jambo walinyosha mikono wengine miwili huku wakisema mabadiliko lazima kwa sauti za chini. 


Rutatina akiomba kura kwa  wajumbe

Viongozi waliochaguliwa ngazi  ya wanawake wa chama hicho  wakipongezwa





Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Joel Kaminyonge, akiwaaga wajumbe  ukumbini, yeye hakugombea kutokana na takwa la katiba ya chama hicho
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho aliyemaliza muda wake Msuya, akitoa jambo ya katika uchaguzi huo


Mwenyekiti Mpya wa Chama hicho, akiomba kura







 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA