SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA UWEZO WA KUKABILIANA NA MAAFA
Na Mwandishu Wetu Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuimarisha uwezo wa nchi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa kutoa mafunzo kwa Timu ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura, inayolenga kuongeza ufanisi wa uratibu na utekelezaji wa hatua za kukabiliana na matukio ya dharura. Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Oktoba, 2026, jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maudhui ya Ndani, Bw. Condrad Millinga, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu wakati akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Jim James Yonazi. Bw. Milinga amesema, mafunzo kwa timu hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha mfumo wa usimamizi wa maafa nchini, hususan katika kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa, taarifa sahihi zinapatikana na tathmini za madhara zinafanyika kwa wakati ili kuokoa maisha, kulinda mali na kupunguza athari kwa jamii. “Timu hii ina majukumu mbalimbali, yakiwemo kushiriki katika operesheni za kuk...