Posts

TANZANIA YAENDELEA KUKUMBUKWA KUHUSU KUPIGANIA UHURU KUSINI MWA AFRIKA

Image
  Makamu wa Rais wa Zimbavwe, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Kembo Mohadi ameendelea kuishukuru Tanzania kwa mchango mkubwa iliyotoa kuzikomboa nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Zimbabwe.  Kanali Mohadi ametoa shukrani hizo Agosti 31, 2025 alipotembelea Chuo cha Wazazi cha Kilimo kilichopo Kaole mjini Bagamoyo ambacho awali kilikuwa Kambi ya wapigania uhuru. “Asante sana kwa kutukomboa, asante sana kwa kutupatia ardhi, asante sana kwa kutuhifadhi. Huu ni ukarimu mkubwa ambao Tanzania mliuonesha bila kujali madhara yake kutoka kwa wakoloni,” alisema Kanali Mstaafu Mohadi. Hata hivyo, Makamu wa Rais Mohadi ametahadharisha kuwa, licha ya Afrika kupata uhuru wa kisiasa lakini uhuru wa kiuchumi bado haujapatikana na ili kufikiwa lazima Afrika iungane kutetea rasilimali zake. Mheshimiwa Mohadi alisema ziara yake katika chuo hicho imelenga kukumbuka hatua kwa hatua, njia walizopitia wapigania uhuru na magumu waliyokumbana nayo ili iwe somo hasa kwa wale a...

ASHA BARAKA KIELELEZO CHA MWANAMKE WA SHOKA KATIKA MUZIKI WA DANS TANZANIA MIAKA 30 BADO NYOTA INAWAKA

Image
NA  SAID MDOE:  Kwa Asha Baraka hakuna adui wa kudumu na ndiyo maana inapotokea msanii wa Twanga Pepeta anahama bendi, bado ataambiwa mlango wa kurejea uko wazi hata kama aliondoka kwa kuchafua hali ya hewa. Asilimia kubwa ya wasanii nyota wa Twanga Pepeta waliohama bendi, walirejea kundini. Sina haja ya kutaja majina ya watu, lakini haihitaji taasisi ya utafiti kubaini kuwa wasanii wengi walioweka alama kubwa Twanga Pepeta, walipojaribu kuhama, walirejea. Jumamosi hii Asha Baraka anakwenda kufanya tukio kubwa la kiburudani pale Brake Point Makumbusho jijini Dar es Salaam. Ni miaka 30 ya Asha Baraka kwenye utumishi wa muziki wa dansi, waimbaji nyota waliowahi kupita kwenye mikono yake kama Nyoshi el Saadat, Ally Chocky, Mwinjuma Muumini na Kalala Jr ambao wote hao kwasasa wanamiliki bendi zao, watasindikiza tukio hilo. Inawezekana Asha Baraka kama binaadamu yeyote yule, ana madhaifu yake, lakini inawezekana pia ana mazuri mengi na anajua namna ya kutengeneza undugu...

MAKAMU WA RAIS WA ZIMBABWE AWASILI NCHINI TANZANIA

Image
  Share Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mheshimiwa Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi amewasili nchini Agosti 30. 2025 kwa ziara ya kazi ya siku mbili hadi Agosti 31 2025 kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Makamu wa Rais Mohadi alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Akiwa nchini, Mheshimiwa Makamu Rais Mohadi atakuwa na mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango Ikulu jijini Dar es Salaam na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari. Aidha, Mheshimiwa Mohadi atatembelea Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha, Chuo cha Kilimo na Mifugo kilichopo Kaole, Bagamoyo na Kituo cha Urithi wa Ukombozi barani Afrika cha jijini Dar es Salaam.                 ...

MAGU WAMWAGIKA MKUTANO WA KAMPENI WA BALOZI DKT. NCHIMBI

Image
  Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia wananchi wa Kisesa na Nyanguge wilayani Magu leo Jumamosi Agosti 30,2025 wakati akielekea mkoani Mara kuendelea na kampeni zake eneo la kanda ya Ziwa ikiwa ni baada ya kumaliza mkoa wa Mwanza. Pamoja na mambo mengine Dkt Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amemnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Kiswaga Destery Boniventura pamoja na Wagombea Udiwani .                    

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Rais wa TLS . Mwambukusi, Jijini Dodoma

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Picha ya pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi, baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 27 Agosti, 2025.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 27 Agosti, 25  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 27 Agosti, 2025.  

CCM YAWASHA MOTO KUSAKA KUONGOZA NCHI KWA MARA NYINGINE

Image
Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiomba Dua pamoja na Wasaidizi wake Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha hicho tarehe 28 Agosti 2025.   @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimezinduwa rasmi kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama hicho CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza uzinduzi huo pamoja na wageni waalikwa akiwemo Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na baadhi ya waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa chama hicho Kabla ya kuelekea katika uwanja wa uzinduzi wa kampeni, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiambatana na wasaidizi wake, alifanya dua maalum Ikulu Jijini Dar es Salaam, ishara ya kumkabidhi Mwenyezi Mungu jukumu zito la kuomba ...