CCM YAWASHA MOTO KUSAKA KUONGOZA NCHI KWA MARA NYINGINE
Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiomba Dua pamoja na Wasaidizi wake Ikulu Jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha hicho tarehe 28 Agosti 2025.











Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimezinduwa rasmi kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama hicho CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza uzinduzi huo pamoja na wageni waalikwa akiwemo Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na baadhi ya waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa chama hicho
Kabla ya kuelekea katika uwanja wa uzinduzi wa kampeni, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiambatana na wasaidizi wake, alifanya dua maalum Ikulu Jijini Dar es Salaam, ishara ya kumkabidhi Mwenyezi Mungu jukumu zito la kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza taifa. Dua hiyo ililenga kuomba baraka, mshikamano na mshindi wa amani katika kipindi chote cha kampeni hadi uchaguzi mkuu.
Uzinduzi huu wa kampeni za CCM ni tukio linalotazamwa na mamilioni ya Watanzania ndani na nje ya nchi, likitarajiwa kuonesha dira na mikakati ya chama kwa miaka mitano ijayo. Aidha, CCM itainadi ilani yake ya uchaguzi ambayo itakuwa dira kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, uboreshaji wa huduma za kijamii, kukuza uchumi na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
Uzinduzi huo pia umehudhuliwa na viongozi wa kitaifa, wanachama wa CCM kutoka mikoa yote ya Tanzania, na wafuasi wa chama hicho. Shughuli hii huashiria rasmi kuanza kwa mbio za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo vyama vyote vitakuwa kwenye kampeni kuomba ridhaa ya wananchi.
Tayari viongozi na wananchi mbalimbali walifurika Kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar el Salaam ili kumsikiliza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi wakati walipowahutibia katika uzinduzi huo wa Kampeni.


Comments
Post a Comment