Posts

WANAHABARI WAPEWA OFFA YA KWENDA KUPATA MAFUNZO JKT

Image
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (kushoto), akiwa ameongozana na mgeni wake , Mkuu wa Jeshi la Kjuenga Taifa  (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele.  wakiwasili katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dodoma  kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari .Akieleza utekelezaji wa majukumu ya JKT na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024,leo Jijini Dodoma Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema azma ya serikali ni kuchukua vijana wote wanaomaliza kidato cha sita ili wahudhurie mafunzo ya lazima,  aidha  kumekuwepo na ongezeko la vijana wanaojiunga na Jeshi kwa mujibu wa sheria kutoka vijana 26,000 mwaka 2022/2023 hadi 52,119 mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54. Ongezeko hilo limepatikana kutokana na jitihada za kuliwezesha jeshi hilo ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024,kiasi cha shilingi bilioni 9.96 kimetengwa ili kuendeleza azma ya kuboresha na kujenga miundombinu makambini...

TUTAZIBORESHA BANDARI ZETU KWA KUZINUNULIA BOTI ZA KISASA ZA UOKOZI -----MKENYENGE

Image
Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw.Kaimu Abdi Mkenyenge  akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/2024 . Wanahabari wakifatilia mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa,akizungumza  na  wanahabari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TASAC na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@     SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)   limesema limejipanga kununua boti tatu za uokozi katika Ziwa Victoria ambazo zitakwenda kusaidia kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza pindi ajali zinapotokea Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Abdi Mkenyenge wakati  akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo w...

BIDHAA MBOVU ZIKAMATIWE VIWANDANI SIYO KWA WALAJI------ DKT. KIJAJI

Image
Waziri wa Viwanda na Biashara DKT. Ashantu Kijaji, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Sita ya Ushauri wa Wakala wa Vipimo nchini  uliofanyika jijini Dodoma leo. Pamoja na mambo mengnine ameitaka bodi hiyo kuhakikisha bisdhaa zinazofikishwa sokoni ziwe na uhakika na siyo kuzikamatia kwenye soko  kama hazina ubora zikamatiwe viwandani zinakozalishwa.  Dkt. Ashatu Kijaji aliyasema hayo wakati akizinduwa bodi   mpya ya ushauri ya Wakala wa Vipimo nchini  na kuendelea kusema ili kuhakikisha walaji wanalindwa kupitia uhakiki wa vipimo pindi  wanaponunua bidhaa mbalimbali   wapate kuona   thamani ya fedha   katika bidhaa wanazonunua.   Dkt.Kijaji ameyasema hayo Jijini Dodoma leo tarehe 27 Julai, 2023 alipokuwa anazindua bodi ya sita ya ushauri ya Wakala wa Vipimo. Aidha, amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala pamoja na wajumbe    kwa kuaminiwa   na kuteuliwa kwani   wanaunda timu bora na inayotoa ...

BANDARI HAIJAUZWA TASAC YATENGA BL.83.1 YA UTEKELEZAJI

    Shirika la Uwakala wa meli Tanzania TASAC  limetenga kiasi cha Shilingi BILONI 83.1 katika kutekeleza  kaguzi mbalimbali , mafunzo na ikiwemo utekelezaji wa miradi kwa mwaka wa fedha 2023-2024 

RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA RASIRIMALI WATU IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu wakati wa hafla ya Chakula cha jioni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023. Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wakielekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 202 Wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi hao wanaoshiriki Mkutano wa Rasilimali watu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Hospitali ya Mombo na tafiti za maambukizi na Usugu wa Dawa za Antibiotic

Image
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf akieleza jambo wakati wa kongamano la mrejesho wa Tafiti za kukinga na kudhibiti maambukizi na Usugu wa Dawa za Antibiotic uliofanyika juzi  kwenye Hospitali hiyo ambalo lilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage ,Picha na kitengo cha Habari Bombo Hospital Katibu Mkuu wa Wizara Dkt Seif Shekalage  kulia akisalimiana na  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa mrejesho wa Tafiti za kukinga na kudhibiti  maambukizi na usugu wa dawa za Antibiotic juzi uliofanyika kwenye Hospitali hiyo kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud