WANAHABARI WAPEWA OFFA YA KWENDA KUPATA MAFUNZO JKT
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (kushoto), akiwa ameongozana na mgeni wake , Mkuu wa Jeshi la Kjuenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele. wakiwasili katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari .Akieleza utekelezaji wa majukumu ya JKT na mwelekeo wake kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024,leo Jijini Dodoma Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema azma ya serikali ni kuchukua vijana wote wanaomaliza kidato cha sita ili wahudhurie mafunzo ya lazima, aidha kumekuwepo na ongezeko la vijana wanaojiunga na Jeshi kwa mujibu wa sheria kutoka vijana 26,000 mwaka 2022/2023 hadi 52,119 mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54.
Ongezeko hilo limepatikana kutokana na jitihada za kuliwezesha jeshi hilo ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024,kiasi cha shilingi bilioni 9.96 kimetengwa ili kuendeleza azma ya kuboresha na kujenga miundombinu makambini.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Gersoni Msigwa, aliwauliza wanahabari ambao wapo tayari kujiunga na Jeshi hilo walinyosha mikono kuashiria wanataka kwenda huko kuchukuwa mafunzo, ndipo alipomuomba Mkuu huyo wa JKT kama kunauwezekana ufanywe utaratibu wa wanahabari wanaotaka nchi nzima waorodheshwe wajiunge,
Mkuu huyo aliwataka wajiandae watakapokuwa tayari wamwambie ili utaratibu uandaliwe kama uliofanyika kwa wabunge, mafunzo hayo ni kwa ajili ya uzalendo na kuipenda kuitumikia nchi na kujenga mwili wako kuwa mkakamavu. Haya wanahabari ambao hamjapitia mafunzo hayo kazi kwenu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Rodney Thadeus, akizungumza kabla ya kumkalibisha Mkurugenzi kwa ajili ya kumkalibisha mkuu wa JKT kuzungumza na wanahabari
Meja Jenerali Mabele na Msigwa wakiteta kabla ya kuanza mazungumzo
Msegwa akimkalibisha Mkuu wa JKT kuzungumza
Wanahabari wakimsikiliza kwa makini
Meja Jenerali Mabele, akizungumza na wanahabari
Comments
Post a Comment