RAAWU WACHAGUANA JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Satadi, Ushauri, Habari na Utafiti (RAAWU), Jane Mihanji, akiongozana na mgeni rasmi katika mkutano wa Chama chake ambaye alikuwa mgeni rasmi Mussa Msumi , Msajili Msaidizi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini. 
Mussa Msami, akitoa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Saba  wa Chama hicho uliofanyika Dodoma leo , amewataka wajumbe wake kuchagua Viongozi ambao hawatakuwa chanzo cha migogoro na Serikali na wafanyakazi wao apamoja na waajili, waendeleze umoja uliokuwepo kabla ya uchaguzi huo. Amewaomba kuwa na mshikamano watumie mda mwingi kukijenga chama  ili kiwe na wananchama wengi. Aidha ameahidi kulifanyika kazi ombi la viongozi wa Chama hicho kuwepo na wimbi la usajili wa vyama ambavyo ving ine vinaudwa kunyanganyana wanachama huku vikitoza ada na michango ya uanachama kidogo  na baadhi ya wafanyakazi waiokuwa na uelewa mpana wanakimbili huko."dhidisheni upendo kwa wanachama wenu muwatumikie vyema  huku mkiwa na ushirikiano na Serikali ya awamu ya Sita mambo yenu yatawanyokea migogoro haijengi bali inabomoa", alisema Mussa.
Mwenyekiti wa RAAWU, Jane Mihanji, akifungua mkutano huo na kuwaomba wajumbe kuchagua viongozi kwa utulivu na baada ya hapo waendelee kuwa na umoja na siyo makundi kama ilivyokuwa wakati wa kuomba kura.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Joseph Sayo akihutubia washiriki wa mkutano huo na kuiomba Serikali kupiti kwa mgeni rasmi kuangalia upya sheria ya usajili wa vyama vya wafanyakazi nchini pamoja na utozaji wa ada za uanachama na kiingilio , alisema kuna vyama vinaanzishwa kwa ajili ya kuwanyanganya wanachama huku wakitumia mwanya wa kutoza ada kidogo za mwenzi na kiingilia na kusababisha kuwa na vyama vingi vya wafanayazi visivyokuwa na tija



Naibu Katibu Mkuu RAAWU, Simon Mbai, akizungumza katika mkutano huo


















 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA