JESHI LA KUJENGA TAIFA LAWAITA VIJANA WA KITANZANIA WA KUZALIWA KUJIUNGA NALO KWA KUJITOLEA

 Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali  Hassan Mabena, akizungumza na wanahabari leo Makao Mkuu ya Jeshi hilo  jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kwa niaba ya  Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Rajabu Mabele, kuhusu kujiunga na jeshi hilo kwa vijana wa kujitolea hususan walio rai wa nchi hii Tanzania Bara na Visiwani.

Brigedia Jenerali Mabena alisema  vijana wanaotakiwa na jeshi hilo ni  vijana wenye Elimu ya Darasa la Saba kuanzia umri wa miaka 16 hadi 18, waliomaliza Elimu ya Msingi kuanzia Mwaka 2022, 2023,2024 na 2025 na awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi.

Aidha kwa vijana wenye Elimu Kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20, waliomaliza Elimu ya Sekondari kuanzia  mwaka 2022,2023,2024 na 2025 na awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari na cheti cha matokeo. 

Aidha alisisitiza kwamba waombaji wa mafunzo hayo wajiepushe na vishoka ambao wamekuwa wakiwadanganya kwamba nafasi hizo kuzipata ni lazima watoe chochote, alisema ni bure haziuzwi, wajiepushe na watu hao anasema hategemea kusikia kijana halisi wa Kitanzania ameingia kwenye mkenge huo akatoa fedha kwa ajili ya kujiunga na jeshi hilo kupata mafunzo ya kujitolea. 

 Pia alisema kutakuwa na mafunzo ya walimu  wa VET Mkuu huyo alisisitiza Jeshi hilo halihusiki na kuwatafutia kazi wahitimu wa mafunzo hayo baada ya kumaliza mkataba wao wa kujitolea amesisitiza wajitokeza kwa wingi wajipatia ujuzi ambao utakuwa dira ya maisha yao




Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo, alipokuwa akiwatangazia mafunzo hayo kwa vijana wa Kitanzania wa kuzaliwa kujiunga na jeshi hilo kujitolea kwa mwaka huu

Baadhi ya makamanda wa Jeshi hilo wakiwa katika mkutano huo





 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA