NMB BUNGE BONANZA KUFANYIKA KESHO JIJINI DODOMA

Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo, akizungumza na wanahabari leo wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo ya Bonanza la NMB Bunge Bonanza litakalofanyika jijini Dodoma kesho, Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika ukumbi wa Spika Dodoma , Bonanza hilo linatalajiwa kuongozwa na Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu. aliwaambia wanahabari benki hiyo imekuwa na kawaida ya kutoa asilimia ya faida yake kwa kutoa huduma kwa jamii na bunge ni sehemu ya jamii hiyo, amewaomba wananchi wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kuja kujionea bonanza la kukata na shoka kesho. Nae Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu uendeshaji wa matamasha ya Bunge Bonanza,  Festo Sanga, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Makete, aliwaambia wanahabri kwamba benki hiyo imekuwa ni mkombozi wa wabunhge wengi ambao hujitokeza kufanya mazoezi kwa kulinda afya za mili yao , alinainisha kwamba kesho kutakuwa na michezo mingi na wamealika Taasisi mbalimbai za serikali kuja kushiriki na washindi watajipatia zawadi mbalimbali. Alitaja baadhi ya michezo ni Mpila wa miguu, riadha, kukimbiza kuku, kukimbia kwa kutumia magunia , mchezo wa bao, chesi, netbo. basket bool nk.








Wakionesha medali ambazo watakabidhiwa washindi
 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA