KATIBU MKUU MSIGWA AKABIDHIWA OFISI ASEMA KAZI IENDELEE

Katibu Mkuu,Wizara ya Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (kushoto), akikabidhiwa  baadhi ya nyaraka za Ofosi ya Msemaji Mkuu wa Serikali aliyekuwa Msemaji ,Balozi Thobias Makoba. Hafla hiyo imefanuyika jijini Dodoma leo.  Kulia kwa Msigwa ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicholaus Mkapa


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicholaus Mkapa,akikabidhi ofisi ya wafanyakazi wa Idara ya Habari - MAELEZO kwa Msigwa

Maofisa wa Wizara mbili wakishuhudia makabidhiano hayo

Hati zza makabidhiano zikisainiwa

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicholaus Mkapa, akisoma hotuba ya makabihdiano,
Kwa niaba ya uongozi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, natoa shukurani kwa viongozi na wafanyakazi wa Idara ya Habari - MAELEZO kwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika ujenzi wa Taifa katika kipindi chote tulichokuwa pamoja.  Tunaikabidhi Idara ya Habari - MAELZO kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambayo sasa ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa na Taasisi zake tatu ambazo ni Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), na Bodi ya Ithibati.


Wanahabari wakishuhudia makabidhiano hayo




Aliyosema Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Balozi Thobias Makoba,
 Nawashukuru sana waandishi wa habari kwa kipindi tulichofanya kazi pamoja na kwa ushirikiano, mmekuwa wazalendo katika utekelezaji wa majukumu yenu, nikitolea mfano wa namna tulivyokesha pamoja kwenye tukio la ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo.
 Naishukuru Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tulifanya kazi pamoja kwa ushirikiano kuanzia viongozi wote hadi wafanyakazi wa ngazi zote.



 Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Gerson Msigwa, alianza akwa kusema
Naamini tutafanya kazi kwa kukidhi matumaini na matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwani ametupa nafasi ya kulitumikia taifa.
 Nawashukuru sana waandishi wa habari wenzangu kwa namna mnavyofanya kazi yenu ya habari kwa nguvu na weledi, naomba tuendelee kushirikiana.
 Nawashukuru viongozi wanaoondoka wanaoniachia kijiti kwa kazi kubwa waliyoifanya, Idara ya Habari - MAELEZO niliyoiacha ni tofauti na ninayoikuta, naahidi na naamini tutasonga mbele zaidi.
 Baada ya Sikukuu za mwisho wa mwaka, nitakutana na waandishi wa habari ili tujipange jinsi tutakavyofanya kazi ili tusonge mbele kwa maslahi ya nchi, kazi yetu sisi waandishi wa habari ni kuilinda Tanzania kwa kalamu zetu.
 Tarehe 19 Desemba, 2024 Jijini Dar es Salaam, nitakuwa na taarifa ya kwanza ya Msemaji Mkuu wa Serikali. Tutazunguza mengi siku hiyo yanayohusu maendeleo ya taifa letu.
Waandishi wa habari tuungane kwa pamoja kuwapa Watanzania taarifa za nchi yetu.
 Nimeambiwa baadhi ya masuala mbalimbali ya waandishi wa habari yanayohitaji kufanyiwa kazi, naahidi kuyashughulikia kwa nguvu kubwa. Ninachoomba ni ushirikiano wenu.

Wanahabri wa Dodoma, wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,kwa kumlejesha Msigwa kuwa chini yao hawakupenda kutajwa majina , walisema kuna mambo ambayo waliyazungumza kwa ajili ya utekelezaji alipoondoka yalikwama hata na baadhi ya mawazo yake yalikwapuliwa yakawa yanafanyika sehemu zingine huku wao wakishuhudia kwa macho."Amelejea bila shaka kazi zitaendelea kama alivyosema ,tunamwamini ni mchapa kazi ni mwenzetu anakulia kwenye taluma hii tumefurahi sana", alisema mmoja wa waandishi.







 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA