WAZIRI KIJAJI AWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YAKE BUNGENI

Waziri wa Uwekezaji, ViwaKinda na Biashara, Dkt. AshatuKijaji,akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni
xii.Kufanya intelijensia ya masoko ya bidhaa na huduma
zinazozalishwa nchini kwenye masoko ya kimkakati;
xiii.Kuingiza orodha ya bidhaa mpya kwenye mfumo na kutanua
mfumo ulioboreshwa kwenye maeneo ya mifugo, uvuvi, madini
yasiyo vito na bidhaa za mbogamboga;
xiv.Kukamilisha Mfumo wa Taarifa za Viwanda (National Industrial
Information Management System – NIIMS) na tathmini ya
viwanda na kuainisha fursa za uwekezaji (Industrial Mapping)
katika kanda ya Ziwa;
xv.Kuimarisha usimamizi wa ubora na usalama wa bidhaa nchini
zikiwemo bidhaa za chakula na vipodozi;
xvi.Kukamilisha uandaaji wa kuzalisha Kinasaba cha Mafuta (Fuel
Marker) nchini; na
xvii.Kuimarisha uwajibikaji wa Wasimamizi wa Ghala kwa
kushirikiana na kampuni za uhakiki wa bidhaa katika ghala.
6. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2024/2025
184. Mheshimiwa Spika; Katika mwaka 2024/2025, Wizara
ya Viwanda na Biashara inaomba Bunge lako liidhinishe jumla ya
shilingi 110,899,722,000 kwa Fungu 44. Kati ya fedha hizo, shilingi
81,115,206,000 ni matumizi ya kawaida, na shilingi 29,784,516,000
ni matumizi ya Maendeleo. Kati ya shilingi 81,115,206,000 za
matumizi ya kawaida, zinajumuisha shilingi 68,352,946,000 fedha
za Mishahara na shilingi 12,762,260,000 kwa ajili ya matumizi
mengineyo.
















 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA