Posts

Showing posts from May, 2024

WABUNGE WAMIMINIKA KUJIONEA MAONYESHO YA WIZARA YA UJENZI

Image
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (kushoto), akitembelea maonyesho ya wizara yake yaliyopo katika viwanja vya bunge,  Wizara hiyo imeandaa maonyesho hayo kuwaonyesha wabunge jinsi ilivyoweza kulejesha usafiri kwa Watanzania baada ya mvua kusomba madaraja na barabara nyingi kuhalibiwa. Hivi sasa zinapitika baada ya watendaji  wa wizara hiyo kukesha saiti Meneja wa Wakara wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Simiyu Boniface Mkumgo(wapili kushoto), akiwaeleza wabunge wa mkoa huo jinsi barabara zinavyopitika kwa sasa baada ya kufanyika matengenezo  makubwa , mvua ilihalibu barabara  nyingi katika mkoa huo. Wa kwanza kushoto ni  Meneja TANROADS mkoa wa Mwanza Ambrosee Pascal ,   

MMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA UJENZI, BARABARA KUPIMWA KWA KUTUMIA MITAMBO------DKT. TULIA ACKSON

Image
SPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia Akson Mwansasu, amepongeza  uwekezaji wa eneo la miundombinu ya Barabara ikiwamo kuiwezesha fedha Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS),kununua mitambo na vifaa vya kisasa hivi karibuni ambapo wakala huo utaisaidia serikali kuondokana na changamoto ya kukabidhiwa miradi ya barabara iliyo chini ya kiwango.  Aidha ameitaka  wizara hiyo  kupitia TANROADS kuhakikisha miradi yote ya  barabara inayokamilia inapimwa ubora kwa kutumia vifaa hivyo vya kisasa kabla mkandarasi kuikabidhi kwa serikali. Akizungumza  Jijini Dodoma wakati akifungua Maonyesho ya siku mbili ya wizara hiyo  na taasisi  zilizo chini yake katika viwanja vya Bunge amesema awali  kulikuwa na matumizi yasiyoridhishwa ya fedha za walipa kodi kutokana na baadhi wakandarasi kukabidhi barabara chini ya kiwango.  Dkt.Tulia aliendelea kusema  kuwa mvua zikinyesha kipindi kimoja zinaweka mashimo na kufanya wabunge kuanza kutafakari namna ya kuishauri, kusimamia kwamba imejengaje barabara

WAZIRI SLAA ALIOMBA BUNGE KUIDHINISHA BAJETI YA WIZARA YAKE TSH. BILIONI 171

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi ,Jerry Slaa, akiwasili bungeni na familia yake kwa ajili ya kusoma hotuba ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2024 na 2025 Akiomba kuidhinishiwa bajerti yake Mkurugenzi Mkuu  wa Shirika la Nyumba  (NHC) Hamad Abdallah, akitambulishwa bungeni Waziri Slaa, akizungumza na wageni wake ambao ni viongozi wa CCM kutoka mkoa wa Dar es salaam baada ya kupiga nao picha   Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Tauhida Cassian-Gallos Nyimbo, akichangia bajeti ya wizara hiyo

WANAVIJIJI WAENDELEA KUJENGA ZAHANATI MPYA ZA VIJIJI VYAO: ZAHANATI MPYA 16 ZINAJENGWA MUSOMA VIJIJINI

Image
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuchangia nguvukazi, fedha taslimu na vifaa vya ujenzi kwenye miradi yao ya maendeleo inayobuniwa na kuanza kutekelezwa na wao wenyewe, ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na shule mpya. Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374. Huduma za Afya Jimboni mwetu: *Zahanati 29 zinatoa Huduma za Afya (25 za Serikali na 4 za Binafsi) *Vituo vya Afya: sita (6) *Hospitali ya Halmashauri/Wilaya: moja (1) Zahanati mpya 16 zinajengwa Jimboni mwetu: Wanavijiji wako kwenye ujenzi wa zahanati mpya kumi na sita (16) kwa kutumia michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kutoka kwa: (i) Kaya za vijijini mwao (ii) Mbunge wa Jimbo (iii) Madiwani na viongozi wengine wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi (iv) Baadhi ya wazaliwa wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi (v) baadae, Serikali Kuu hutoa michango ya kusaidia ukamilishaji wa zahanati zinazojengwa na wanavijiji. Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura: Kijiji cha Ka

MAJALIWA ATAKA WAVAMIZI WA ARDHI KUCHUKULIWA HATUA KAMA JINAI NYINGINE

Image
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (kushoto) na Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga wakielekea kwenye uzinduzi wa Klinik ya Ardhi katika viwanja vya Bunge tarehe 23 Mei 2024.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya TMRC wakati wa maonesho ya Klinik ya Ardhi katika viwanja vya Bunge tarehe 23 Mei 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah (kushoto) wakati wa maonesho ya Klinik ya Ardhi katika viwanja vya Bunge tarehe 23 Mei 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akipata m

YANGA WALITEKA BUNGE SHANGWE KILA KONA AZIZ KII NA GAMONDI WAWA KIVUTIO

Image
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro, akisoma hotuba ya bajeti ya wizara yake huku akishuhudiwa na wachezaji wa timu ya yanga na viongozi wake walipotinga bungeni, ilikuwa ni shangwe walipowasili asubuhi na walipotambulishwa ndipo kila kona ya ukumbi ilikuwa shangwe  mpaka pale Naibu Spika Azan Zungu,aliyekuwa akiliongoza bunge alipowaomba wabunge waliowapenzi na wanachama wa yanga kupunguza kushangilia. Wakipiga picha na wabunge huku wakionyesha mkono mitano tena na timu zitaendelea kupigwa hivyo hivyo Rais wa Klabu hiyo na kocha wakiongozakuingia ukumbini, huku mfanyakazi wa bunge Kizingiti (kushoto) akishuhudia