MMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA UJENZI, BARABARA KUPIMWA KWA KUTUMIA MITAMBO------DKT. TULIA ACKSON
SPIKA wa Bunge, Dkt. Tulia Akson Mwansasu, amepongeza uwekezaji wa eneo la miundombinu ya Barabara ikiwamo kuiwezesha fedha Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS),kununua mitambo na vifaa vya kisasa hivi karibuni ambapo wakala huo utaisaidia serikali kuondokana na changamoto ya kukabidhiwa miradi ya barabara iliyo chini ya kiwango.
Aidha ameitaka wizara hiyo kupitia TANROADS kuhakikisha miradi yote ya barabara inayokamilia inapimwa ubora kwa kutumia vifaa hivyo vya kisasa kabla mkandarasi kuikabidhi kwa serikali.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua Maonyesho ya siku mbili ya wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake katika viwanja vya Bunge amesema awali kulikuwa na matumizi yasiyoridhishwa ya fedha za walipa kodi kutokana na baadhi wakandarasi kukabidhi barabara chini ya kiwango.
Dkt.Tulia aliendelea kusema kuwa mvua zikinyesha kipindi kimoja zinaweka mashimo na kufanya wabunge kuanza kutafakari namna ya kuishauri, kusimamia kwamba imejengaje barabara kama hiyo.
"Tunafahamu miaka miwili iliyopita Rais Dk Samia alipewa tuzo katika eneo la miundombinu ya barabara bila shaka tuzo ile inaonesha namna ambavyo tumepiga hatua," amesema.Bajeti ya Wizara hiyo inatalajiwa kusomwa na Waziri wake Inoncent Bashungwa kesho.
Wabunge wakiwa katika maonyesho hayo
Mbunge akipewa zawadi na Mfanyakazi wa TIB
Mbunge Profesa Sospiter Muhongo, akipata maelezo kutoka kwa mtendaji mkuu wa TAMESA
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa,akimkalibisha Spika kufungua maonyesho hayo
Comments
Post a Comment