WANAVIJIJI WAENDELEA KUJENGA ZAHANATI MPYA ZA VIJIJI VYAO: ZAHANATI MPYA 16 ZINAJENGWA MUSOMA VIJIJINI
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuchangia nguvukazi, fedha taslimu na vifaa vya ujenzi kwenye miradi yao ya maendeleo inayobuniwa na kuanza kutekelezwa na wao wenyewe, ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na shule mpya.
Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.
Huduma za Afya Jimboni mwetu:
*Zahanati 29 zinatoa Huduma za Afya (25 za Serikali na 4 za Binafsi)
*Vituo vya Afya: sita (6)
*Hospitali ya Halmashauri/Wilaya: moja (1)
Zahanati mpya 16 zinajengwa Jimboni mwetu:
Wanavijiji wako kwenye ujenzi wa zahanati mpya kumi na sita (16) kwa kutumia michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kutoka kwa:
(i) Kaya za vijijini mwao
(ii) Mbunge wa Jimbo
(iii) Madiwani na viongozi wengine wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi
(iv) Baadhi ya wazaliwa wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi
(v) baadae, Serikali Kuu hutoa michango ya kusaidia ukamilishaji wa zahanati zinazojengwa na wanavijiji.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura:
Kijiji cha Kaburabura ni moja ya vijiji vitatu (3) vya Kata ya Bugoji. Vijiji vyote vitatu vinatumia zahanati moja iliyoko Kijijini Bugoji.
Umbali mrefu wa kutembea kwenda kupata Huduma za Afya, ni moja ya sababu kuu iliyosababisha Kijiji cha Kaburabura kiamue kujenga zahanati yake.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alipiga Harambee ya kupata fedha na vifaa vya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho. Taarifa ya matokeo ya Harambee hiyo ilishatolewa, na inapatikana kwenye Tovuti ya Jimbo la Musoma Vijijini ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Michango inakaribishwa:
Wadau wa Maendeleo wanakaribishwa sana kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura - tafadhali tuma fedha zako za mchango kwenye Akaunti ya Kijiji:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300684
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kaburabura
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Wanakijiji wa Kaburabura wakichangia nguvukazi zao kwenye ufyatuaji wa matofali ya ujenzi wa zahanati ya kijiji chao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 23.5.2024
Comments
Post a Comment