PROFESA ALOYCE MAYO ATUHUMIWA KUTAPELI ENEO LA HEKA TATU DAR

 Zaina Mohammed,akiwaonyesha waandishi wa habari mabaki ya nyumba yake iliyopo Kunduchi Mtongani eneo la Mbuyuni  baada ya  kuvunjwa na mabausa na Askari Polisi wa kituo cha Wazo Hill  waliotumwa na tajili yao anayedaiwa mhadhili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitengo cha Uhandisi  Profesa Aloyce Mayo. Ameomba wasamalia wema wamsaidie kwani anataka kutapelewa eneo lake  lenye ukubwa wa hekal 2 Mtoto wake amepigwa hadi mimba ya miezi saba kuharibika. Amemuomba Rais Dk. John Magufuli, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamsaidia pia hata wanasheria wanawake kipigo anachokipata kutoka kwa hao wanaotumwa na profesa huyo anajiona kama yupo nchi isiyokuwa yake, inadaiwa hata Wizarani Profesa huyo anakesi nyingi za nyumba. Hata walinzi wa amani nao wanatumiwa na dhulumati huyo Kituo cha Polisi Wazo Hill kimegeuka pango la walanguzi wametumiwa kuja hapo kumpiga na kumtisha ahame  eti hawezi kushindana na tajili bora akubali kuondoka.




 Akionyesha sasa kimebaki kifusi tu hivi sheria ipo wapi inayompa mwenye fedha kutapeli maeneo ya wasiokuwa na fedha



 Mchanga na kokote ameweka katika eneo hilo ili aanze ujenzi kwenye eneo lisilokuwa lake
 Hiki ni kibanda ambacho amejenga kinatumiwa na mabausa na askari polisi wa Wazo Hilli kujihifadhi wakiwa kwenye dolia yao ili wasinyeshewe na mvua
 Eneo lenyewe lilivyo
 Godoro linalotumiwa na walinzi kujipumzishia kukiwa na joto  kwenye kibanda
 Zaina Mohammed,akiweka tandiko lake vizuri kandokando mwa barabara ya Kunduchi Mtongani eneo la Mbuyuni amekuwa akilala hapo na familia yake miezi miwili sasa baada ya nyumba yake kuvunjwa na mabausa na Askari Polisi wa kituo cha Wazo Hill  waliotumwa na tajili yao anayedaiwa mhadhili wa chuo Kikuu cha Dar es SalaamKitengo cha Uhandisi  Profesa Aloyce Mayo. Ameomba wasamalia wema wamsaidie kwani anataka kutapelewa eneo lake Mtoto wake amepigwa hadi mimba ya miezi saba kuharibika



 Magari yakipita huku akijilalia eneo hilo ni hatari kwa maisha yake mama huyu


Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA