HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI FREEMAN AIKAELI MBOWE
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni Freeman Mbowe, akisoma Hutuba yake leo bungeni
HOTUBA YA KIONGOZI
WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA
BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17.
Inatolewa
chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo
la Januari, 2016
_________________________________
1. SHERIA YA
UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF MINISTERIAL
FUNCTIONS – ACT, 1980.
Mheshimiwa
Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa
muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.
Inasomeka
ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published in the
Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility
for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to
any minister and may in that notice specify the effective date of the
assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika,
mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi
kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za
Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa
kisheria.
Mheshimiwa Spika,
mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument)
unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe
17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo,
majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:
§ Coordination
of Government Business
§ Leader
of Government Business in the National Assembly
§ Link
between Political Parties and Government.
§ National
Festivals and Celebration of Management of Civic Contingencies (relief).
§ Facilitation
and Implementation of Plans for the Development of Dodoma as Capital of
Tanzania.
§ Coordination
and Supervision of Transfer of the Government to Dodoma.
§ Government
Press Services.
§ Investment,
Economic Empowerment, Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation
Policies and their Implementation.
§ Facilitation
of the Development of Informal Sector.
§ Performance
Improvement and Development of Human Resources under this Office
§ Extra
– Ministerial Department, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects
under this Office.
REGIONAL
ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:
§ Decentralization
by Devolution (D by D), Rural Development, Urban Development Policies and their
Implementation.
§ Regional
Administration.
§ Primary
and Secondary Education Administration
§ Dar
Rapid Transit – DART.
§ Performance
Improvement and Development of Human Resources under this Office.
§ Extra-Ministerial
Departments, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under
this Office.
Mheshimiwa Spika, kitendo
cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina maanisha kwamba
majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa mwaka 2010,
kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.
2. UVUNJWAJI WA
KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA SERIKALI
Mheshimiwa Spika,
hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha
Bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa Spika,
Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge
hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya
fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa
madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.
Mheshimiwa
Spika
utaratibu huu unatiliwa nguvu na
Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001(
Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali
kuleta Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya
Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Mheshimiwa Spika, utaratibu
huo wa kisheria umekuwa ukivunjwa na
Serikali kwa kufanya matumizi ya fedha
ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka ya Bunge
ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Mheshimiwa Spika, ili
kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa
na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha
2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6
Mheshimiwa
Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara
ilikuwa imeshapokea kutoka hazina
shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika,
ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na
hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na
Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya
nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya
2015 au sheria ya Fedha ya 2015.
Mheshimiwa Spika, kitendo
cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge
ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.
3. UHURU NA
MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE
Mheshimiwa Spika,
Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja Bunge
kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na
madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali
isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali
imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana
kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.
Mheshimiwa Spika,
Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua
Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao
iwapo hawafanyi kazi inavyostahili.
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka
wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni
kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya
kujitegemea.
Mheshimiwa Spika,
Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza
fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali
mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa
katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu
matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu
masuala muhimu kwa jamii,
Mheshimiwa Spika, katika
Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki
uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa Spika,
Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika
mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa
kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo
basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.
Mheshimiwa
Spika, naomba kuwasilisha.
Freeman Aikaeli
Mbowe (Mb)
KIONGOZI
WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI
MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA
OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

Comments
Post a Comment