MSIBA WA MAX NA MATUKIO MBALIMBALI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
 Vijana wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Jijini Mwanza, Juni 26,2015, kundelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na Uhai wa Chama mkoani Mwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Juni 27, 2015 kwa ajili ya kushiriki shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Chadema Wilaya ya Magu, Juliana Kachiru, akikabidhi kadi na 'magwanda' ya chama hicho kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahan Kinana, baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa, Kisesa, akiwa katika ziara ya kikagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Magu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete,  akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Magu Mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wa Dkt. Bilal, wakati walipokuwa katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mlongo akijadili jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Anthony Diallo, wakati wa Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika  katika Uwanja wa Mkapa, jimbo la Magu mkoani Mwanza
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Bilal, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na baadhi ya Viongozi wakijumuika na waombolezaji katika shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Vijana wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Jijini Mwanza, Juni 26,2015, kundelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi na Uhai wa Chama mkoani Mwanza
 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Katibu kuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka maji katika dumu, alipozindua mradi wa maji wa safi na salama katika eneo la Ibadanja, akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama Magu mjini, katika jimbo la Magu mkoani Mwanza, 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Magu, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza
 Makamu akiifariji famiia ya marehemu Max
Katibu wa CCM, Kinana, akiwahutubia wanaccm wilayani magu
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji matofali, alipofika kukabidhi vufaa vya ufyatuaji matofali kwa kikundi cha kufyatua matofali kwa kutumia teknolojia rahisi na ya kisasa na nafuu katika eneo la Nyigogo, Magu mjini akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionyeshwa chanzo cha Maji cha mradi wa maji wa Nyanguge, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Magu mkoani Mwanza


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiongoza mazoezi ya Jogging, yaliyoandaliwa na Vijana mkoani Mwanza leo Juni 27, 2015, kwa lengo la kujenga mwili na kukuza mshikamano miongoni mwa vijana hao. Kinana na Nape wapo mkoani humo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili viwanja vya Ikulu jana kuhudhuria katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad wakiwa  katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais,(kushoto) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji
 Viongozi mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais wakiwa katika futari ya pamoja iliyotayarishwa jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
 Wafanyakazi wanawake wa Wizara mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais wakiwa katika futari ya pamoja iliyofanyika jana katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi Wakuu wa Nchi walihudhuria ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa Kwanza wa Pili  wa Zanzibar  Balozi  Seif Ali Iddi

Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar pia walijumuika katika futari ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais,iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA