TAASISI ya Brien Holden Vision yatoa misaada Mkuranga
Afisa
Mkazi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute
Eden Mahayo, akizungumza wakati alipofika katika hospitali ya
Wilaya ya Mkuranga kukabidhi msaada wa vifa vya macho kwa ajili ya
wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao
watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.Kulia ni Mganga mkuu wa
Wilaya hiyo Dk.Francis Mwanisi,Kaimu Mkurugenzi wa Mkuranga Mbenjamin
Majoya na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho Dk.Nkundwe Mwakyusa.Mkazi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo kushoto) akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto)akimuonyehsa mashine ya kutengenezea miwani baada ya kukmkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Mbenjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya Wilaya hiyo.kulia ni Mratibu huduma za macho mkuranga dkt.Gilbert Mrema.
Afisa
Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute
Eden Mahayo (kushoto) akijaribu kumpima miwani matroni wa Hospitali
ya Mkuranga Rosemary Magombola wakati wa hafla ya kumkabidhi wa msaada wa
vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili
ya kuwahudumia wanafunzi wa shule za msingi 122 za mkuranga ambao
watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na
matibabu bure. Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Kaimu
Mbenjamin Majoya (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya hiyo Dkt,Francis Mwanisi
Matroni wa haospitali ya wiraya ya Mkuranga Mkuranga Rosemary Magombola akisoma moja ya maneno kwenye kibao maarumucha kupimia macho mara baada ya kukabidhiwa msaada huona taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden kwa ajili ya wanafunzi wa shuleza msingi 122 .Kulia ni Mratibu wa taifa wa huduma za macho Dkt.Nkundwa Mwakyusa (kushoto) Mratibu wa mradi huo kwa watoto wa shule za msingi toka taasisis ya ya Brien Holden Vision Institute Eden ,Rebecca Kasika.
Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa kibaha mkoa wa pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden Mahayo (kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi wa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa Wilaya hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure
Wafanyakazi wa hospitali ya Kibaha kitengo cha macho wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa ya Brien Holden Vision Institute Eden,mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4.
Wafanyakazi
wa Hospitali ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi
isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute Eden, mara baada ya
kukabidhiwa msaada wavifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4
kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi ambao watanufaika na mradi huo bure.
TAASISI
isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision imetoa msaada wa vifaa vya
kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za Mkuranga na
Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa msada huo ,Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo
Benjamin Majoya alisema msaada huo utasaidia katika
kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi katika Wilaya
hiyo kutokana na idadi ya watoro darasani kupungua kuanzia
mwaka huu.
Alisema
kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na kuongezeka kwa
kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu yasekondari mwaka ujao.
Majoya
alisema msaada uliotolewa na Taasisi hiyo umekuja kwa wakati
mwafaka kwa wakati amabo ulikuwa ukihitajika hivyo mbali ya kuwasaidia
wanafunzi wa shule za msingi lakini pia utawasaidia wananchi wote wa
Wilaya hiyo.
Alibainisha
kuwa msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia macho pamoja
kutengenezea miwani za aina mbalimbali utasaidia kuondoa tatizo la
uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu kwamba huenda
watoto wao wamerogwa .
Akielezea
ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa sababu ya mwanafunzi
kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa mara hivyo kusababisha
utoro.
“Tunaishukuru
sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada waliotupatia na
tunaahidi kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie kwamba hii itabaki
kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ’”alihitimisha Majoya.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden Mashayo alisema lengo
la Taasisi yake ni kuwajengea uwezo wa kuona wanafunzi pamoja na walimu
lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu ili waweze kuwapima
wanafunzi wapate huduma stahiki ili kuondokana na tatizo hilo..
Mashayo
aliahidi ushirikiano baina ya Taasisi yake ,Wizara ya Afya,Wilaya ya
mkuranga na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila mwezi mara mbili
ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana na tatizo la
uoni hafifu ambalo litapungua kwa asilimia 10 .
Kwa
upande wake Mkuu wa Mratibu wa huduma za macho Taifa kutoka Wizara ya
Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa mradi huo unaosaidia shule za
Msingi bagamoyo na Kibaha umeshahudumia shule 121 katika awamu ya
kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 .
Akizungumzia
changamoto zinazowakabili alisema kuwa huduma hizo hazipewi
kipaumbele kwasababu serikali inajua tu kunawafadhili .
Hata
hivyo alibainisha kuwa ili kutatuua changamoto hizo na kuifanya
jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa ya macho mikakati iliyopo
huenda mambo yakabadilika na mwaka huu jamii itaanza kupata taarifa
sahihi kuhusu magonjwa ya macho.
Naye
daktari Mtalamu wa macho Gilbert Massawe wa hospitali ya wilaya ya
Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji waliishukuru
Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya
Brien
Holden Vision kwa msaada wao na kubainisha kuwa utasaidia kupunguza
idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.


Comments
Post a Comment