MAHAFALI CHUO CHA UDAKTARI ZANZIBAR
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume na Mkewe Mama Shadya Karume (chini)
wakisalimiana na walimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Vingozi mbali mbali alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyojumisha jumla ya wahitimu 35
Wahitimu wa Mafunzo ya Udaktari wakiwa katika maandamano wakati wa Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais akienda kuwatunuku wahitimu
Wakisimama wima wakati wimbo wa taigfa ulipokuwa ukipigwa
Walimu Madaktari Bingwa katika Chuo cha Madaktari Zanzibar kutoka Nchini CUBA wakiitikia Wimbo wa Taifa lao ulipopigwa leo katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo hicho
Walimu Madaktari Bingwa katika Chuo cha Madaktari Zanzibar kutoka Nchini CUBA wakiwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume na Mkewe Mama Shadya Karume (kulia) pamoja na Viongozi wengine Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakiwa katika Mahfali
Wageni waalikwa waiwa katika mahafali hayo
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania Jorge Luis Lopez Tormo alipokuwa akitoa salama zake wakati wa Mahfali
Wahitimu wa Mafunzo ya Udaktari wapatao 35 yaliyotolewa na Mataktari Bingwa kutoka Nchini CUba wakila kiapo cha Utii wa kazi zao mbele ya Rais
Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN Ulpiano Perez kutoka Cuba akimtunuku shahada Yassin Khamis Mohamed akiwa ni miongomi mwafunzi 35 waliohitimu mafunzo ya Udaktari katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Yussuf Said Ahmed baada ya kumtunukia shahada ya Udaktari wakati wa Mahfali ya kwanza ya Chuo
Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN Ulpiano Perez kutoka Cuba akimtunuku shahada Zena Kassim Mohamed
Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake
Waziri wa Afya Rashid Serif Suleiman akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wanachuo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa zawadi kwa Fatma Mrisho Haji akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora waliopata zawadi katika Mahfali ya Kwanzaya chuo hicho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa zawadi kwa mwanafunzi bora zaidi ya wote walimaliza masomo ya Udaktari Nadhira Suleiman Said
Rais Shein, akihutubia
Comments
Post a Comment