Posts

SERIKALI KUANZISHA MAMLAKA YA MILKI TANZANIA

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wizara ya Ardhi na kampuni zinazojihusisha na mipangomiji, upimaji ardhi na uendelezaji wa milki nchini kilichofanyika tarehe 23 Novemba 2026 jijini Dar es Salaam. Na Munir Shemweta Serikali iko mbioni kuanzisha Mamlaka ya Milki Tanzania kwa lengo la kuimarisha usimamizi, udhibiti na uendelezaji wa sekta ya milki nchini. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, amebainisha hayo leo Novemba 23, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kazi cha Wizara ya Ardhi na kampuni zinazojihusisha na mipangomiji, upimaji ardhi na uendelezaji wa milki nchini. Amesema, Serikali inahitaji kuwa na chombo chenye mamlaka kamili ya kisheria kitakachoweza kusimamia na kuendeleza sekta ya milki ili kuhakikisha inakuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa taifa. Kwa mujibu wa Waziri huyo, kwa sasa Serikali hainufaiki kikamilifu na sekta ya milki kutokana n...

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AMTEMBELEA MKUU WA KWANZA WA MAJESHI WA JWTZ

Image
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,W Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe  22 Novemba, 2026, amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa kwanza wa Majeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  (JWTZ), Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya (Mstaafu), nyumbani kwake Tengeru, mkoani Arusha. Katika ziara hiyo, Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Rhimo Nyansaho amepata fursa ya kufanya mazungumzo na Jenerali Sarakikya, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mawasiliano na ukaribu na kiongozi huyo aliyewahi kuliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Waziri wa Ulinzi na JKT  kumtembelea Jenerali Sarakikya, jambo linaloonesha mwendelezo wa mawasiliano na kutembeleana kati yao. Ziara hiyo pia imetoa fursa ya Waziri kupata nafasi ya kuzungumza na kiongozi huyo mstaafu na kumtambua kwa nafasi yake ya kihistoria katika uongozi wa JWTZ. Waziri huyo makini amekuwa akifanya kazi bila kuchoka akifanya kazi za wizara huku akiwatembelea makamanda waliowahi kulion...

UCHAGUZI WA SHIRIKISHO TUCTA KUFANYIKA DODOMA 25 NA 26 MWEZI HUU

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho Huru la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Aloysius Mapembe (kushoto) akiwa na  Katibu  wa Kamati hiyo Gerald Shayo (katikati) na Prosper Mutungi, wakizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma kuwaelezea taratibu za uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unaotalajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dodoma katika ukumbi wa Mabeyo. Viongozi hao wamewaomba wanaohusika na uchaguzi huo wakiwemo wagombea wanaotalajiwa kufikia 100 kuwepo Dodoma kama walivyosema. Viongozi hao walisema kumekuwepo na maneno ya mitaani kuhusu ,kuahilishwa uchaguzi huo wamefafanua kwamba hizo ni hadhithi za mitaani na hapa chini ni taratibu za uchaguzi huo na nafasi za wagombea   

WAJUMBE RAAWU WAMPA JANE MIHANJI MITANO TENA

Image
Wagombea nafasi ya Uenyekiti Chama cha  Raawu, Jane mihanji (katikati) na Benjamin Magori (kulia) wakipiga kura katika uchaguzi huo ambapo  baada ya kutopata kura nyingi ikabidi waludie wawili hao na badae kura zilipohesabiwa Jane alishinda kwa kura 59 kwa kura 52 alizopata Magori  Wagombea w a Nafasi hiyo walikuwa watano mmoja akajitowa Mwenyekiti kwa miaka mitano tena Jane Mihanji, akiwashukuru wajumbe wapigakura  baada ya kutangazwa mshindi kwa mara ya pili kuoingoza Raawu, uchaguzi huo ulimalizika asubuhi leo na ulianza saa tatu asubuhi jana  Mihanji akitangaza kuachia ngazi na viongozi wenzake wote ili kupisha uchaguzi mkuu uanze kufanyika Mihanji akitoa ufafanuzi akiwa kama mjumbe wa kawaida  katika mkutano huo Wagombea nafasi ya Mwenyekiti wakipita mbele ya wajumbe kabla ya kuanza kuomba kura mmoja mmoja Jane Mihanji, akiomba kura Wajumbe wakipiga kura  

MARAIS DKT.SAMIA NA MUSEVENI WAZINDUA KIWANDA CHA MAGARI NCHINI UGANDA

Image
    Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikata utepe pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, kama ishara ya uzinduzi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akivuta kitambaa pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, kama ishara ya uzinduzi Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026.  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda, wakitembelea Kiwanda cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Mpigi nchini Uganda, tarehe 19 Novemba, 2026. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na Rais...

RAAWU WACHAGUANA JIJINI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Satadi, Ushauri, Habari na Utafiti (RAAWU), Jane Mihanji, akiongozana na mgeni rasmi katika mkutano wa Chama chake ambaye alikuwa mgeni rasmi Mussa Msumi , Msajili Msaidizi wa Vyama vya Wafanyakazi nchini.  Mussa Msami, akitoa hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Saba  wa Chama hicho uliofanyika Dodoma leo , amewataka wajumbe wake kuchagua Viongozi ambao hawatakuwa chanzo cha migogoro na Serikali na wafanyakazi wao apamoja na waajili, waendeleze umoja uliokuwepo kabla ya uchaguzi huo. Amewaomba kuwa na mshikamano watumie mda mwingi kukijenga chama  ili kiwe na wananchama wengi. Aidha ameahidi kulifanyika kazi ombi la viongozi wa Chama hicho kuwepo na wimbi la usajili wa vyama ambavyo ving ine vinaudwa kunyanganyana wanachama huku vikitoza ada na michango ya uanachama kidogo  na baadhi ya wafanyakazi waiokuwa na uelewa mpana wanakimbili huko."dhidisheni upendo kwa wanachama wenu ...