RAIS WANGU DKT.SAMIA SULUHU HASSAN NAOMBA UTENGE MUDA WAKO UFUATILIE SAKATA HILI C W T
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@ RAIS wangu Dkt. Samia Suluhu Hassan, mtoto wako akikunyea mkono unaukata, hebu tenga muda wako mfupi fuatilia Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kisichoisha migogoro, kinapata mchango mkubwa wa ruzuku unaofikia Sh. Bilioni 4 Kila mwezi kutoka Serikalini. Kunamadai wasaidizi wako hizo fedha wanazimezea mate ndiyo maana ugomvi haushi hapo. Wanachofanyiwa walimu ni sawa yanayofanyika katika Halmashauri nchini wakurugenzi wanakwapua fedha kwasabau wanaelewana na wakurugenzi. Wakurugenzi wanahamishwa kwenda kituo kingine cha kazi baada ya kukwapua mamilioni ya shilingi wabunge wanalalamikia wakurugenzi hao lakini hatua hazichukuliwi kwa sababu wanakula na wakubwa waliopo wizarani. Rais wangu mimi siyo mtetezi wa Maganga na wenzake lakini walichofanyiwa ni unyanyasaji mkubwa walikamatwa katika mkutano wa kamati kuu wa kupanga matumizi ya chama. Haya wakati yanatokea kulikuwa na kutoelewana kati ya katibu mkuu na Mwenyekiti wa kikao...