DKT. BITEKO AMWAKILISHA RAIS SAMIA UWEKAJI WAKFU ASKOFU MPYA JIMBO KATOLIKI BUKOBA
📌 Asema Nchi inajivunia Haki, Uhuru, Umoja na Amani Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, leo amemwakilisha Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kuwekwa Wakfu na Kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Jovitus Mwijage ikiwa ni tukio la kihistoria kutokana na kupita takriban miaka 50 kutoka kufanyika sherehe kama hiyo ya uwekaji wa wakfu. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Kaitaba wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa na Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato. Akitoa Salam za Dkt. Samia kwa waumini na wananchi waliohudhuria sherehe hizo, Dkt. Biteko ameeleza kuwa, Rais ataendelea kutoa ushirikiano kwa Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ili kwa pamoja walete maendeleo nchini. Amesema, Rais anatambua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali nch...