Posts

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK.HUSSEIN MWINYI AMEJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA MASHINDANO MAKUU YA 8 YA TAJWEED QURAN

Image
SHARE WASHIRIKI wa Mashindano ya 8 ya Tajweed Quran Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani) akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Masjid Noor Muhammad Kwa Mchina Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, yaliyoandaliwa na Taasisi Majlisil Quran Zanzibar(Picha na Ikulu)/ JAJI Kiongozi wa Mashindano Makuu ya 8 ya Tajweed Quran Zanzibar akitowa maelezo kwa washiriki wa mashindano hayo kabla ya kuaza, yaliyofanyika katika Masjid Noor Muhammad kwa Mchina Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Majlisil Quran Zanzibar.(Picha na Ikulu) MSHIRIKI wa Mashindano ya 8 ya Tajweed Quran Zanzibar.Ustadh Hamad Juma Salum, akishiriki katika mashindano hayo na kuibuka mshindi wa kwanza, yaliyofanyika katika Masjid Noor Muhammad kwa Mchina Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Maljisil Quran Zanzibar.(Picha na Ikulu) WAUMINI wa Dini ya Kiisla...

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2023. Wajumbe wa Kamati pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye uzinduzi wa Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2023. ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Wajumbe wa Kamati ya kufanya tathmini ufanisi wa Utendaji Kazi wa Wizara hiyo ya Mambo ya Nje mara baada ya uzinduzi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya p...

MHANDISI LUHEMEJA: KULINDA RASILIMALI ZA MAJI NI MUHIMU SANA KATIKA NCHI

Image
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuendeleza na kutunza rasilimali za maji hapa nchini ni jambo la msingi na lenye faida kubwa kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo kama moja ya urithi katika jamii. Amesema hayo katika kikao cha Bodi ya Maji ya Taifa mkoani Morogoro na kusisitiza kwa wajumbe wa bodi hiyo kutumia uzoefu wao katika kutoa majibu ya changamoto zinazohusu maji na sio kuegemea katika mabadiliko ya tabianchi kwa sababu miradi ya maji inategemea uwepo wa vyanzo vya maji muda wote Mhandisi Luhemeja amesema mabadiliko ya hali ya hewa yatumike kubuni mbinu za kuhakikisha maji yanakuwepo nchini, na kuongeza hivi sasa mpango ni kuwa na gridi ya maji nchini, ambayo itaimarisha huduma ya maji katika maeneo yenye upungufu. Ameitaka Bodi ya Maji ya Taifa kutembelea wadau na kuona changamoto zao ili kupata majibu, kufanya tathmini na kushauri ipasavyo kwa sababu huduma ya maji maana yake ni kuangalia uhai wa Watanzania. “Tuwe na ...

NMB BONGE LA MPANGO – ‘MTO ULE ULE YAZINDULIWA WATEJA KUVUNA MIL. 180/

Image
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe. Paul Chacha pamoja na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi wakipeperusha bendera kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule, katika uzinduzi uluifanyika katika soko  la Buhongwa jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki ya NMB, Wogofya Mfalamagoha, wapili kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Aikansia Muro na kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa – Ladislaus Baraka. Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB – Filbert Mponzi (wapili kushoto) akimfungulia akaunti ya NMB dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza wakati wa kuzindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango – Moto Uleule. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Misungwi – Mhe. Paul Chacha (pili kulia). Mkuu wa Wilaya ya Misungwi – Paul Chacha akimkabidhi kadi ya benki dereva bodaboda katika soko la Buhongwa jijini Mwanza, baada ya kumfungulia akaunti ya NMB...

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe.David Concar, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-3-2023.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania.Mhe David Concar , mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-3-2023.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. David Concar alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 30-3-2023, kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAANDALIZI YA DIRA MPYA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 YAANZA NCHINI

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Christian Omolo ,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Aprili 3, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma. SOMA ZAIDI HAPO CHINI Kamishna wa Idara ya Mipango ya Taifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Aprili 3, 2023, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma. Baadhi ya Wakuu wa Idara na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa karibu mkutano na waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya...

NAMIBIA YAVUTIWA NA TANZANIA INAVYOKABILIANA NA TATIZO LA AJIRA

Image
UJUMBE wa Bunge la Namibia umeimwagia sifa Serikali ya Tanzania namna ilivyojipanga kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana kupitia programu zinazotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Kiongozi wa ujumbe huo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge hilo ya Rasilimali watu na Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mbunge, Mhe. Nono Katjingisua, ametoa pongezi hizo leo Machi 30, 2023 baada ya kukutana na Mofisa wa Ofisi hiyo wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii, Festo Fute. Mhe.Katjingisua amesema Serikali ya Namibia mwaka 2022 ilikumbwa na tatizo la ajira kwa vijana hivyo hali hiyo imewasukuma kuja Tanzania kujifunza namna inavyokabiliana na tatizo hilo. “Tumepata maelezo ambayo na sisi tutakaporejea bungeni tutazingatia kama vile kuwa na program ya taifa ya kukuzaji ujuzi ili kuwajengea uwezo vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri au kuajiriwa kulingana na mahitaji ya s...