MAANDALIZI YA DIRA MPYA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 YAANZA NCHINI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Christian Omolo ,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Aprili 3, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma. SOMA ZAIDI HAPO CHINI

Kamishna wa Idara ya Mipango ya Taifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Aprili 3, 2023, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa karibu mkutano na waandishi wa habari kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Aprili 3, 2023, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.



Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Christian Omolo (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu hafla ya uzinduzi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Aprili 3, 2023, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.
Naimu Katibu Mkuu, akijibu maswali ya wanahabari
Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu

 Ndugu wanahabari, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia
uzima na afya njema inayotuwezesha kuendelea kutekeleza majukumu yetu
kwa weledi na hivyo kuchangia katika juhudi za Serikali za kupata maendeleo
na kujenga ustawi wa Taifa. Vile vile, niwashukuru nyie pia kwa kuitikia wito
na kuwa tayari kuhabarisha umma kuhusu tukio hilo adhimu.
2. Ndugu wanahabari, tumekusanyika hapa leo kwa lengo la kupeana taarifa
muhimu juu ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (Tanzania
Development Vision 2050 – TDV 2050). Dira hii itatoa maono na kuweka
malengo ambayo Taifa letu linataka kuyafikia ndani ya kipindi cha miaka 25
ijayo baada ya kuisha kwa kipindi cha utekelezaji wa Dira tuliyo nayo sasa ya
Taifa ya Maendeleo 2025. Maandalizi ya Dira mpya ya 2050 yanakidhi matakwa
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndio mwongozo
mkuu wa nchi yetu.
3. Ndugu wanahabari, Historia ya upangaji wa mipango nchini imeanza kuanzia
nchi ilivyopata uhuru ambapo matamanio yalikuwa juu ya kupambana na
ujinga, umaskini na maradhi. Katika kuhakikisha azma hii inafikiwa,
kuliandaliwa mipango ya vipindi tofauti tofauti. Mwaka 1964, Tanzania
ilifanikiwa kuandaa Mpango wa kwanza wa Muda Mrefu wa miaka 15 ambao
ndani ya utekelezaji wake uliimarishwa na Azimio la Arusha la mwaka 1967.
Mpango wa Pili wa Muda mrefu uliandaliwa Mwaka 1981 ambao ulipangwa
kutekelezwa kupitia mipango minne (4) ya miaka mitano (Five Year
Development Plan’s). Utekelezaji wa mipango hii ulienda sambamba na
utekelezaji wa programu mbalimbali zilizosimamiwa na Shirika la Fedha
Duniani (IMF) na Benki ya Dunia (WB) zilizokuwa na lengo la kuleta utulivu wa
kiuchumi na marekebisho ya kimuundo chini.
4. Ndugu wanahabari, Katika muktadha huo wa kufanikisha malengo
yaliyopangwa, Serikali ilianza mchakato wa maandalizi ya Dira ya Maendeleo
ya Taifa (TDV 2025) mwaka 1995 ambao ulikamilika mwaka 2000. Utekelezaji
wa Dira hii ulianza kupitia programu za kupunguza umaskini ambapo
programu ya kwanza ilikuwa ni Mkakati wa Kupunguza Umaskini (PRS I)
mwaka 1999/2000 hadi 2002/03, mkakati wa pili kutoka 2004/05 hadi 2009/10
ambao pia unajulikana kama Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umaskini (MKUKUTA I), na Mkakati wa tatu ulitelezwa kuanzia
mwaka 2010/11 hadi 2014/15, ambao ulijulikana kama MKUKUTA II
3
5. Ndugu wanahabari, katika mwaka 2009/10, Serikali ilifanya tathmini ya
utekelezaji wa Dira 2025 kupitia mikakati na programu za maendeleo. Tathmini
hii ilibainisha uhitaji wa Taifa kuanza kupanga vibaumbele vya nchi. Suala hili
lilipelekea kuandaliwa kwa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu
(LTPP) 2011/12 - 2025/26). Mpango huu wa miaka 15 ulipangwa kutekelezwa
kwa mipango ya muda wa kati ya miaka mitano (5) na mipango ya muda mfupi
ya mwaka mmoja (1).
6. Ndugu wanahabari, Katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya
Mwaka 2025, Taifa limeweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja
mbalimbali hususan za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, utekelezaji wa
Dira 2025 unafikia tamati mwaka 2025. Kwa msingi huo, ni jukumu letu sote
kwa nafasi zetu kuanza kufikiria juu ya mafanikio ya utekelezaji wa dira 2025 na
mustakabali wa nchi yetu katika miaka ya mbele ijayo.
Taja mafanikio hapa ya TDV 2025
7. Ndugu wanahabari, Kwa msingi huo, Serikali imeanza mchakato wa kuandaa
Dira Mpya ya Maendeleo 2050. Hivyo, naomba kuchukua fursa hii kuwapa
taarifa na kuwaalika nyinyi pamoja na watanzania wote kwa ujumla katika
uzinduzi rasmi wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
utakaofanyika tarehe 03 Aprili, 2023 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention
Centre kuanzia saa 02:00 asubuhi. Niwaombe mtumie nafasi zenu kuhahikisha
ujumbe huu unawafikia watanzania wote na ni matumaini yangu kuwa
mtatumia nafasi zenu katika kujenga uelewa kwa watanzania juu ya umuhimu
wa Dira ili kuwezesha kuwa na Dira ya Watanzania.
8. Ndugu wanahabari, ili kufanikisha zoezi la maandalizi ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050 kunategemea kwa kiasi kikubwa ushiriki wa wadau wote.
Hivyo, nitoe rai kwa wadau wote katika maeneo yao kushiriki kikamilifu katika
kutoa mchango wao utakaowezesha kuandaliwa kwa Dira yenye maono ya
watanzania kwa miaka 25 ijayo.
9. Ndugu wanahabari, napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru sana kwa
kutenga muda wenu kuja kunisikiliza. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali,
suala hili ni muhimu sana kwa Taifa na nimatarajio yangu kuwa mtaendelea
kulipa uzito na kipaumbele katika shughuli zenu. Aidha, naomba kusisitiza juu
ya kufikisha taarifa za uzinduzi maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya 2050
utakaofanyika tarehe 03 Aprili, 2023 na ambapo Mgeni rasmi Mhe. Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Phillip I. Mpango
Asanteni San

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA