MKURUGENZI DUWASA AKUTANA NA WANAHABARI WA DODOMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, akizungumza na wanahabari wa mkoa wa Dodoma akiwaeleza mkakati wa Mamlaka yake kuhusu kuwahudumia wananchi wa jiji la Dodoma. Mkutano huo umefanyika leo. Mkurugenzi amebainisha kwamba kunawizi mkubwa wa mita za maji zaidi ya 100 zimeibiwa mwezi huu, inadaiwa zinaenda kuyeyushwa na kutengenezwa bangili na zingine kuuzwa kama vyuma chakavu. anawaomba wananchi ambao ni wateja wao wazijengee mita zao au wazifunge ndani ya fensi lakini kwa masharti ya kutoigusa,wawasaidie kusoma mita hiyo kuhakikisha inafikiwa na msomaji wa mamlaka hiyo ili wawahudumie vyema jambo jingine kuwahakikishia wasoma mita usalama wao kuna wateja wengine wakienda kusoma mita wanawafungulia mbwa. Kuna wizi mkubwa wa mifuniko ya chemba za maji machafu zinaibiwa na kupelekwa kuuzwa kama vyuma chakavu amewaomba wananchi na wafanyabishara kuwa wazalendo kwa kutonunua mifuniko hiyo kwani mingi ina nembo ya mamlaka hiyo (nchi hii ni yetu sote hasa makao makuu Dodoma tuwe wazalendo kuwa walinzi wa vifaa vya umma kwani vinanunuliwa kwa kodi ya wananchi, tuwakamate wanaohujumu miundombinu hii tutawapa zawadi kubwa watakaofanya hivyo", ameomba Mkurugenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Rahel Alex Muhando, akimkalibisha Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo. Rahel aliwaambia wanahabari kwamba mamlaka ya maji mkoani Dodoma ni yao hawana bundi kuisaidia kuhabarisha matatizo ambayo yanatokea mitaani ambapo wao wanachelewa kuyaona ili wawatumikia vyema wananchi wa jiji la Dodoma .
Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi

Comments
Post a Comment