KATIBU MKUU TUGHE AWAASA WATUMISHI WA CHAMA HICHO
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Rugemalira Rutatina, (pichani). amewaasa watumishi wa Chama hicho kuanza kufikili kwa kina namna watakavyo watumikia wanachama na wananchi katika kufanya juhudi za kuongeza wanachama,
akizungumza kwa mara ya kwanza kama katibu Mkuu wa Chama hicho katika mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho lililoambatana na kuwachagua manaibu katibu wakuu wawili , wajumbe kamati kuu na wadhamini wa chama.
Rugemalira Rutatina alisema hakutakuwa na kisingizio cha mtumishi kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa kisingizio cha makundi ya kampeni za uchaguzi uliomalizika
amesema baada ya uchaguzi kumalizika makundi yote yamevunjwa sasa ni mwendo wa Ali mpya na Kasi Mpya "tulikuwa na makundi katika kampeni za uchaguzi mimi sitapenda kulaumiwa kwamba nimemchukulia hatua mtumishi kisa hakuwa upande wangu tukachape kazi bila woga", alisema
Nae Mwenyekiti mpya wa Chama hicho Aloyce Mapembe, akifungua Mkutano wa Baraza hilo aliwahakikishia wajumbe wa Mkutano huo kuwa atakiongoza chama hicho kwa haki na hataweza kumuonea mtu yoyote ataendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na upngozi uliopita uku akimwagia sifa kedekede mwenyekiti aliyemaliza muda wake kwa kujenga jengo jipya la kisasa la chama hicho, imebakia kazi ndogo ya kulimalizia.
aidha amewaomba wanachama washikamane katika kuendelea kukijenga chama kwani wamekikuta chama kipo sehemu nzuri hakuna haja ya kukidhoofisha hivyo ni wakati wa kuchapa kazi kwa sasa.
Mwenyekiti Mpya wa Chama hicho Aloyce Mapembe, akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho leo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi na maarifa na siyo kwa mazoea
Wagombea nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho wakiomba kura kwa wajumbe
Comments
Post a Comment