eRITA YAWAPIGA MSASA WABUNGE YARAHISISHIA WANANCHI UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII.


Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa kielektroniki wa eRITA, unaolenga kupunguza muda, gharama na urasimu katika upatikanaji wa huduma.

Mfumo huo unawezesha mchakato mzima wa huduma kuanzia maombi, uhakiki wa taarifa na nyaraka, uchakataji, malipo hadi utoaji wa huduma au nyaraka husika. Huduma zinazopatikana kupitia eRITA ni pamoja na usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, vifo, ndoa na talaka, pamoja na huduma za bodi za wadhamini.,

Viongozi  wa wakala hao waliwapatia mafunzo hayo wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ambapo waliwasifia wakala hao kwa hatua hizo ambazo zinawafanya wananchi wawe na elimu ya uandikaji wa wosia kabla ya kifo na kuacha familia zikitapeliena na hata watoto kukosa haki zao kutokana na baadhi ya wasimamizi kutokuwa waminifu.

Miongoni mwa maboresho yaliyofanyika ni uhakiki wa papo kwa papo wa vyeti vya kuzaliwa na vifo, malipo kwa kutumia kadi za benki, marekebisho ya vyeti kupitia mfumo, pamoja na wananchi kupata taarifa za hatua ya maombi yao kupitia ujumbe wa simu au akaunti zao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maboresho hayo yameongeza wigo wa wananchi kupata huduma wakiwa ndani na nje ya nchi, kuokoa muda na gharama, kurahisisha ufuatiliaji wa maombi na kuimarisha ubadilishanaji wa taarifa kati ya taasisi za Serikali na sekta binafsi.

RITA pia imeeleza kuwa matumizi ya eRITA yamechangia kuimarisha usalama wa kumbukumbu, uwazi na uwajibikaji, huku yakipunguza utegemezi wa mifumo ya karatasi na kuwezesha upatikanaji wa takwimu muhimu kwa ajili ya mipango na maamuzi.

Katika mafanikio yake, RITA imeeleza kuwa imepata tuzo ya Mradi Bora wa TEHAMA katika Sekta ya Umma kwenye kipengele cha kupunguza urasimu, huku mwaka wa fedha 2025/2026 ikiingia katika taasisi 10 bora zilizofanya maboresho katika matumizi ya mifumo ya kidijitali na utoaji wa huduma.

RITA imeahidi kuendelea kuboresha eRITA, kuwekeza katika miundombinu ya TEHAMA, kuimarisha usalama wa taarifa, kutoa mafunzo kwa watumishi na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya mfumo huo.







Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Edwin Swale, ambaye pia ni Mbunge wa Lupembe, akifungua warsha ya mafunzo hayo leo bungeni

 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA