MEJA JENERALI MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KANEMBWA

    Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, akikagua Paredi ikiwa ni ishara ya kuhitimisha mafunzo ya JKT kwa vijana wa Kundi la Mujibu wa Sheria, Operesheni Linda Amani, na Kundi la Kujitolea, Operesheni Nishati Safi.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema somo la Uzalendo na Uzalendo wa Kidijitali kwenye silabasi za mafunzo ya JKT litaendelea kuboreshwa zaidi ili kuelimisha vijana umuhimu wa kutumia vema mitandao ya kijamii.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Septemba 18, 2026 wakati akifunga ukurasa wa zoezi la uhitimishaji wa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Linda Amani na Kujitolea Operesheni Nishati Safi katika Kikosi cha Kanembwa JKT kilichopo mkoani Kigoma.

Katika hatua nyingine, Meja Jenerali Mabele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa katika kuboresha miundo mbinu ya Vikosi vyake ili liweze kutoa mafunzo kwa vijana wengi wa Kitanzania.
Zoezi la ufungaji wa mafunzo ya JKT kwa vijana Kundi la Lazima (Mujibu wa Sheria) Operesheni Linda Amani na Kundi la Kujitolea Operesheni Nishati Safi lilianza Septemba 8, 2026 ikiwa ni mara ya kwanza kwa makundi hayo mawili kufanya mafunzo na kuhitimishwa kwa pamoja.

Akishuhudia askari hao wakionyesha mambo waliyojifunza








 

Comments

Popular posts from this blog

AJIRA MPYA 41,500 SERIKALINI ZATANGAZWA KATIBU MKUU UTUMISHI JUMA MKOMI

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA