WAZIRI MAKONDA AFIKISHA UJUMBE WA RAIS DKT.SAMIA KWA RAIS WA CAF DKT. MOTSEPE
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Paul Christian Makonda amekutana na Rais wa Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motsepe Jijini Rabat, Morocco na kukabidhi barua kutoka kwa Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pamoja na kukabidhi barua hiyo Mheshimiwa Makonda aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa amemhakikishia Dkt. Motsepe kuwa Rais Samia yupo tayari wakati wote kushirikiana na CAF katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kandanda ikiwemo mashindano mbalimbali. Amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika maandalizi ya kuwa wenyeji wa AFCON 2027 sambamba na Kenya na Uganda na kwamba imedhamiria kuonesha tofauti kubwa na mashindano yaliyopita. Aidha, Makonda amemuomba Dkt. Motsepe kuiangalia Tanzania kimkakati ili mipango inayowekwa na Serikali ipate mafanikio makubwa yanayotarajiwa. Kwa upande wake Dkt. Motsepe amemshukuru Rais Sa...