MARUFUKU MWANAFUNI KUCHAPWA AU KULEJESHWA NYUMBNANI KISA MICHANGO YA SHULE----WAZIRI MKEND

Waziri wa ‎Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza ahadi za Rais Samia kwa vitendo, hususan kumlesha mwanafunzi nyumbani kisa kakosa mchango wa shule

Waziri Mkenda amesema nikosa kubwa  kwa mwalimu yeyote atakayemlejesha mwananfunzi nyumbani au kumchapa bakola kisa kakosa  mchango wa shule

Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jijini Dodoma, katika kutoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Rais samia ndani ya siku 100.

Amenainisha kwamba Serikali inasema Elimu hailipiwi ili watoto wa kitanzania wote wasome , hata hivyo amesema kamati za shule zinaweza kuwa na utaratibu wao wa kuchangia kama chakula kwa wananfunzi wao 

Hata nhivyo siyo mwanafunzi kuchapwa au kulejeshwa nyumbani kisa mzazi hajatoa fedha za mchango huo,amesema sasa amechoka kusema hivyo sasa ataanza kiuwachukuliamhatua walimu wanaofanya nhivyo.

Mkenda amewaagiza Wakurugenzi nchini kuwafatilia walimu wa namna hiyo ambao wanawasumbuwa wanafunzi ili kukomesha tabia hiyo kwani kunamadai baadhi wanaacha fule kisa michango hiyo.

"Kunamichango mingine ya kujipati fedha ,lakini kama ni ya chakula mzazi anatakiwa kulipa kwani hiyo inaidhinishwa na kamati ya shule kwenye mikutano yao na siyo kuwa na michango mingi, ashughulikiwe mzazi na siyo mtoto',amesema Waziri Mkenda 

‎Pia ameongeza kuwa utekelezaji wa ahadi za Rais unaenda sambamba na upanuzi wa fursa za elimu kupitia utoaji wa mikopo na ujenzi wa miundombinu ya elimu ya juu, ambapo amesema kuwa Tanzania inaendelea kujenga kampasi mpya 16 za vyuo vikuu katika mikoa ambayo awali haikuwa na kampasi hizo.

‎Amebainisha kuwa mikoa yote nchini tayari ina vituo vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, huku ujenzi wa kampasi mpya ukiendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo kampasi ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) mkoani Kigoma na Kagera pamoja na kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mkoani Lindi, ambapo jiwe la msingi tayari limewekwa.











 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.