Kwagilwa awataka watumishi wa umma kuheshimu na kuzingatia muda wa kazi
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amewataka watumishi wote walio chini ya Ofisi hiyo kuripoti kazini saa 1:30 asubuhi na kutekeleza majukumu yao hadi saa 9:30 alasiri kama ilivyoanishwa katika Kanuni F.1 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009. Kwagilwa am etoa maelekezo hayo leo tarehe 24 Novemba, 2025 baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Kisasa jijini Dodoma majira ya saa 1:30 asubuhi na kubaini idadi kubwa ya walimu wa shule hiyo hawajaripoti kazini kwa wakati ili kutekeleza wajibu wao kama ilivyokusudiwa na Serikali. “Wakati nimefika hapa nimekagua kitabu cha maudhurio ya walimu na kubaini walimu 16 tu kati ya walimu zaidi ya 55 ndio waliowahi kazini, hivyo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mhe. Profesa Riziki Shemdoe ninaelekeza kuwa, watumishi wote walio chini ya OWM- TAMISEMI wakazingatie muda wa ...