KASIMAMIENI UBORA WA ELIMU KWA WACHINI YENU UTENDAJI UWE MZURI---PROFESA SHEMDOE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI),  Profesa. Riziki Shemdoe, amewataka wakuu wa shule za msingi nchini  kufanya kazi kwa upendo huku wakiwasimamia walimu waliochini yao kufanya kazi kwa amani na mshikamano ili kuhakikisha huduma ya elimu na ubora wake unaacha  tabasamu  kwa wanafunzi nchini. Waziri huyo ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa UMOJA wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA), unaofanyika jijini Dodoma.

TAMISEMI ni kuwatumikia watanzania hivyo kila aliyebahatika kupata nafasi ya uongozi ahakikishe anawatumikia watanzania kwa ufanisi na uzalendo.

“Sisi watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI tunao wajibu wa kipekee wa kuleta tabasamu kwa wananchi, tukitimiza kikamilifu jukumu la kutoa huduma bora,” amesema Profesa. Shemdoe.

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu. Atupele Mwambene amesema, Walimu Wakuu walioudhuria mkutano huo ndio wenye jukumu la kupeleka tabasamu kupitia malezi watakayoyatoa kwa walimu wanaowasimamia na hatimaye wanafunzi watapata uelewa na ufaulu mzuri.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Didas Bambaza amemuahidi Profesa. Shemdoe kuwa, Walimu Wakuu watakwenda kutekeleza kwa vitendo maelekezo yote aliyoyatoa ili huduma zitakazotolewa katika shule zote zilete tabasamu kwa wanafunzi na wananchi.

Kaulimbiu ya Mkutano Mkuu huo wa Saba wa Mwaka wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi (TAPSHA) ni Mtaala Ulioboreshwa kwa Elimu Bora; Ujuzi na Ubunifu kwa Maendeleo endelevu ya Taifa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Reuben Kwagilwa, akisisitiza jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti wa UMOJA wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Tanzania Bara (TAPSHA),Rehema Ramole  akizungumza katika mkutano huo

 
Wanachama wa umoja huo wakisikiliza hotuba za viongozi kwa umakini mkubwa














Waziri na naibu wake wakiteta





 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.