WAZIRI MAVUNDE AAGIZA LESENI 73 ZA UTAFITI WA MADINI NCHINI ZIFUTWE


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameiagiza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 73 za utafutaji na uchimbaji wa kati wa madini, kutokana na maeneo husika kutokuendelezwa kama sheria inavyotaka.
Akizungumza na wanahabri Leo Jumanne jijini Dodoma huku akiwa ameambatana na Naibu waziri wa wizara hiyo Dkt Steven Kiruswa, Waziri Mavunde amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya baadhi ya wamiliki wa leseni kushindwa kurekebisha makosa yaliyobainishwa na Tume ya Madini, licha ya kupewa muda wa kufanya hivyo na wasifanye .
Amesema kuwa wamiliki wa leseni 44 za utafutaji wa madini pamoja na wamiliki wa leseni 29 za uchimbaji wa kati wameshindwa kutekeleza masharti ya leseni zao na hivyo kukiuka sheria ya madini nchini .
Waziri Mavunde amewataka wamiliki wote wa leseni za madini kuhakikisha wanazingatia matakwa ya sheria na masharti ya leseni wanazomiliki, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia tabia ya watu kuchukua leseni na kisha kushindwa kuyaendeleza maeneo husika na baadae inapotokea kuvamiwa na wachimbaji wengine kuanza kulalamika.
Amesema “Sitawavumilia watu wanaochukua leseni na kukaa nazo bila kuziendeleza, naielekeza Tume ya Madini kusimamia sheria kikamilifu, kutoa hati za makosa kwa wote wanaokiuka masharti, na kufuta leseni zote zisizoendelezwa bila kumuonea mtu yoyote.”
Ikumbukwe, Aprili mwaka huu, Wizara ya Madini ilitangaza mpango wa kufuta leseni za kampuni mbalimbali, hususani kubwa, ambazo kwa muda mrefu hazikuendeleza maeneo yake na baada ya hatua hiyo, kampuni nyingi ziliwasilisha taarifa za utetezi, na nyingine tayari zimeanza kurejesha shughuli za uchimbaji.





Wanahabari wakiwajibika kwa waziri Mavunde








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIOPITA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.