Mkuu wa Wilaya ya Same Aeleza Jitihada za Kuendeleza Utalii na Uhifadhi

NA ASHRACK MIRAJI Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda J. Mgeni, amefungua milango ya maendeleo ya utalii kwa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Nkoba Mabula, leo Septemba 25, 2024. Katika mkutano huo, Mgeni alisisitiza kwamba utalii si tu fursa ya kiuchumi, bali pia njia ya kuboresha maisha ya wananchi na kuhifadhi mazingira, huku akielezea jitihada za kutangaza vivutio vya wilaya ili kuvutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa eneo hilo. āHapa Same tumezungukwa na hifadhi mbalimbali na kutambua umuhimu wa uhifadhi, mwaka huu tulifanya tamasha kubwa la Same Utalii Festival. Tamasha hili liliwakutanisha wadau mbalimbali, na wananchi wameweza kuona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na wanyamapori,ā alisema Mgeni. Aliongeza kuwa tamasha hilo lilikuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha jamii kuhusu faida za uhifadhi na jinsi unavyoweza kuchangia katika ustawi wa kiuchumi. Mgeni alitoa shukrani kwa Rais kwa kuendelea kutekeleza sera za maendeleo ya utalii, akieleza kuw...