WAZIRI BASHE AWAPASHA WADAU WA TASINIA YA MBEGU

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, akizungumza katika mkutano wa wadau wa Tasnia ya Mbegu nchini katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma leo

Waziri wa kilimo Husein Bashe, amewataka wazalishaji wa mbegu za kilimo nchin kukusanya taarifa zao za uzalishaji ndani ya masaa 24 na kuzipeleka katika Taasisi ya kudhibiti ubora wa  mbegu nchini watakaopuuza agizo hilo watafutwa katika orodha ya wazalishaji nchini

Agizo hilo amelitoa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanunuzi wa mbegu nchini katika mkutano wa wadau wa Tasinia ya mbegu katika mkutano wa kusikiliza kelo na adha wanazopata katika biashara hiyo

Akiongea kwa ukali Waziri Bashe aliwataka wazalishaji hao kuwa makini na uzalishaji  kwani hataki tena kusikia wakulima wakilima  wanapotegemea kupata mavuno bora wanaambulia kupata hasara kwa kuuziwa mbegu feki.

Tasinia ya kilimo siyo kificho cha makanjanja wa kuuza mbegu feki, amewambia hakuna majadiliano atakaepuuza atapoteza kazi kama mfanyakazi wa wizara hiyo.

Aliwambia kulikuwa na tatizo la mbolea feki hivi sasa limeisha kwa kuwa na mfumo mzuri wa kuuza mbolea hizo kila mkoa na kodi namba yake.

Wapo katika mpango wa kubadilisha sheria  kuanzia mwakani haitaruhusiwa kuuza duka la dawa za kilimo kama muuzaji hajasomea uuzaji huo kwa shughuli za kilimo lazima awe na kisomo cha kuanzia awe na elimu ya Diploma ,shahada na kuendelea.
 Haiwezekani dhana za kilimo kuuzwa na mtu asiyekuwa na elimu ya kilimo na dawa zake ."Hatutaki makanjanja kwenye kuuza bidhaa za kilimo, kila mtu anayefdeli katika maisha anakimbilia kuja kwenye kuwapiga wakulima kwa kuwauzia bidhaa fiki, stakubali kama mimi nitaendelea kuwa waziri katika wizara hii, labda mwakani wananchi wa nzega waninyime kura  na Waziri asiniteua kuwa Waziri",Alisema Waziri Bashe.
Aidha naye  Mkurugenzi wa  Taasisi ya udhibiti wa ubora  mbegu Patrick Bodiagi, alisema bado wanakabiliwa na changamoto za wazalishaji kutokuwa na elimu ya kutosha kukabiliana na utengenezaji wa mbegu bora.

Akwilini Makata wa Karanosi Amcos, akizungumza katika mkutano huo alimuomba Waziri bashe kuwasaidia wao kama wauzaji wa dawa za kilimo na pembejeo zake wamekuwa wakipata wakati mgumu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya kuuza vyakula vya binadamu wanauza bidhaa wanazouza wao na hawakamatwi.

Matuyani Loipotoki Laizel, ambaye ni msambazaji wa bidhaa za kilimo, alimpongeza Waziri Bashe kwa kuwa mkali kwa wale ambao wanacheza na zana za kilimo ambapo kilimo ni uti wa mgongo katika nchi hii.







Wadau wa mbegu  za pembeje wakiwa katika mkutano huo















Akwilini Makata wa Karanosi Amcos, akizungumza katika mkutano huo alimuomba Waziri bashe kuwasaidia wao kama wauzaji wa dawa za kilimo na pembejeo zake wamekuwa wakipata wakati mgumu kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya kuuza vyakula vya binadamu wanauza bidhaa wanazouza wao na hawakamatwi.
















Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza  Waziri Bashe kwa makaini

Mfanyabishara Laizel, akibadilishana mawazo na Waziri Bashe

Waziri akitoka mkutanoni


 

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA