Posts

Showing posts from October, 2024

KATIBU MKUU MAJI AFUNGUA KIKOA CHA WATENDAJI MAMLAKA ZA MAJI

Image
  Share Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefungua kikao cha Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, jijiji Dodoma kilichohusu kupokea na kujadili maelekezo ya viongozi wa Wizara ya Maji. Miongoni mwa masuala yaliyowekewa mkazo katika kikao hicho na Mhandisi Waziri ni pamoja na ushirikiano kwa watendaji katika kutimiza majukumu yao ili kuleta matokeo chanya na ushirikishwaji wa wananchi na viongozi kuhusu huduma za maji zinazotolewa.

WAZIRI SILAA AZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 436.4 MKALAMA

Image
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa, leo Oktoba 24, 2024, amezindua mradi wa maji  na Zahanati yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 436.4 katika wilaya ya Mkalama, mkoani Singida. Mradi wa maji uliozinduliwa katika kijiji cha Nkalakala, umegharimu shilingi milioni 348.9  na unapunguza changamoto waliyokuwa nayo wananchi ya  kutembea umbali mrefu kutafuta maji. Meneja wa RUWASA wilaya ya Mkalama, Mhandisi Christopher Saguda, alisema tanki hilo lina uwezo wa lita 90,000 litaweza kuhudumia vituo 12 vya kuchotea maji, huku ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 100. Mradi mwingine uliozinduliwa na Waziri Silaa ni zahanati ya Igonia iliyopo kijiji cha Mtogo Mwili uliogharimu shilingi Milioni 87.4 ambao ulianza kutekelezwa kwa michango ya wananchi kabla ya Serikali kuendeleza ujenzi wake. Zahanati hiyo itahudumia vijiji vya Igonia, Ikungu, na Mtamba, ikinufaisha wananchi 1,408 kulingana na sensa ya 2022. Huduma zitakazotolewa ni pamoja na

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yakutana na maofisa wa Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii

Image
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timoth Mzava akibadilishana mawazo na wasaidizi wa kamati yake kabla ya kikao kuanza leo jijini Dodoma amabapo alikutana na Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA, Tanapa na Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji wa Nyuki Tabora  (BTI) Maofisa  wa Wizara hiyo na Taasisi zake  

MWENYEKITI MWANYIKA APONGEZA TBS NA CAMARTEC

Image
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Jafo (kulia), akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, alipokuwa akifungua kikao cha Idara mbili za Wizara yake ambazo ni Shirika la Viwango nchini (TBS) na  Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, akifungua kikao hicho, ambapo alizipongeza taasisi hizo ambazo  zinagusa maisha ya moja kwa maja ya wananchi wa Tanzania na kuwaomba watendaji wake kuwa makini zaidi kusikiliza malalamiko ya wananchi  na kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka, ili kumsaidia Rais DKT, Samia Suluhu Hassan, ambaye moyo wake ni kuona wananchi wanapata huduma zilizo bora. · Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Dkt. Ashura A. Katunzi, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti huyo Mkurugenzi Mkuu wa   Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC, Godfrey Mwinama, a

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAINYOSHEA KIDOLE DART

Image
: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia Serikali za Mitaa,  Justin Nyamoga, akisisitiza jamnbo alipokuwa akizungumza na vingozi wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar es Salaam (DART),mbela ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo Zainabu Katimba Naibu Waziri TAMISEMI, Zainabu Katiba (kushoto), akiwa na viongozi wa DART mbele ya  wajumbe wa kamati hiyo waliofika hapo leo Naibu Waziri Katimba, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati hiyo