KATIBU MKUU MAJI AFUNGUA KIKOA CHA WATENDAJI MAMLAKA ZA MAJI

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amefungua kikao cha Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, jijiji Dodoma kilichohusu kupokea na kujadili maelekezo ya viongozi wa Wizara ya Maji.
Miongoni
mwa masuala yaliyowekewa mkazo katika kikao hicho na Mhandisi Waziri ni
pamoja na ushirikiano kwa watendaji katika kutimiza majukumu yao ili
kuleta matokeo chanya na ushirikishwaji wa wananchi na viongozi kuhusu
huduma za maji zinazotolewa.
Comments
Post a Comment