Posts

Showing posts from June, 2024

DC SAME MKOANI KILIMANJARO ATOA NENO KWA WANANCHI WAKE

Image
RUNGU LA DC SAME KUWASHUKIA WAZAZI WANAOTUMIA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO KAMA MTAJI KULIPANA FEDHA. Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe. Kasilda Mgeni amewaonya baadhi ya wazazi wanaotumia kesi za ukatili wa kijinsia kwa watoto kama mtaji kulipana fedha pindi anapofanyiwa ukatili kuacha mara moja tabia hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea kuathiri saikolojia na afya ya mtoto pamoja na kumfanya ashindwe kutimiza ndoto zake. Ameeleza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi uliofanyika Kata ya Mamba Myamba, ambapo amewasisitiza wananchi hao kutowaficha watuhumiwa wa vitendo hivyo kwenye jamii ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki. “Niwaombe sana wazazi muwalinde watoto wenu, jengeni urafiki na watoto wenu ili waweze kuwaambia madhara ambayo wanayapata huko njiani wanapoenda shule na kurudi watawaambia, na bahati mbaya sisi wazazi hatuwafuatilii watoto tupo bize na kilimo cha tangawizi hatuna muda wa kukaa na watoto wetu w

WAZIRI MKUU MAJALIWA AAHIRISHA BUNGE NA KUSEMA BILIONI 346 KUTUMIKA KUIMARISHA USALAMA WA MILKI ZA ARDHI -

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imesaini mkataba wa sh. bilioni 346 na Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ambao unalenga kuimarisha usalama wa milki za ardhi na kuwezesha miundombinu ya usimamizi wa ardhi nchini. Amesema mkataba huo uliosainiwa Februari, 2022 ni wa mradi ambao unatekelezwa kwa miaka mitano (2022/2023 - 2026/2027) katika Halmashauri 67 na Mikoa 26. Mradi huo una vipengele vinne ambavyo ni kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa njia ya urasimishaji kwa kutoa Hatimiliki 1,000,000 katika maeneo ya mijini na Hatimiliki za Kimila 500,000; kuimarisha mifumo ya taarifa za ardhi; kujenga miundombinu ya ardhi; na usimamizi wa mradi.   Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Juni 28, 2024) wakati akitoa hotuba ya kuahirisha mkutano wa 15 wa Bunge jijini Dodoma.  Bunge limeahirishwa hadi Agosti 27, mwaka huu. Akielezea mradi huo, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Juni 15, mwaka huu, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na u

MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ANENA NA WANAHABARI JIJINI DODOMA

Image
YALIYOJIRI LEO JUNI 27, 2024 JIJINI DODOMA KWENYE MKUTANO WA MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO) NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI BW. THOBIAS MAKOBA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAAZIMIO YA MKUTANO WA WAZIRI MKUU NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NCHINI # Kwa takribani siku nne sasa kumekuwa na majadiliano kwa ngazi mbalimbali kati ya serikali na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara hapa nchini. Mazungumzo haya yalitokana na madai na hoja takribani 41 ambazo wafanyabiashara waliziwasilisha serikalini ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kutokana na hoja hizo, na baada ya vikao na mawaziri wa sekta husika, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia falsafa ya R 4 za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa ile ya Reconciliation kwa maana ya maridhiano, Leo tarehe 27 Juni, 2024 amehitimisha mazungumzo hayo jiji Dodoma. # Mheshimiwa Majaliwa, kwa niaba ya Serikali kwa pamo

Bendera ya Taifa yapeperushwa vema Nchini Rwanda.

Image
Kikundi cha Maafisa na  Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Vyombo vya Usalama na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoshiriki Zoezi la 13 la Medani la Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki "FTX Ushirikiano Imara 2024" lililofanyika nchini Rwanda,  kimekabidhi bendera ya taifa mara baada ya kurejea nchini tarehe 23 Juni 2024. Akizungumzia kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda, Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Iddi Said Nkambi  amewataka Maafisa na Askari walioshiriki zoezi hilo kutumia vizuri mafunzo waliyoipata kwenye zoezi hilo  pindi wanapotakiwa kukabiliana na matishio ya kiusalama na Majanga mbalimbali yanayoweza kutokea nchini, nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla. Naye Kamanda Kikosi cha JWTZ wa zoezi hilo Luteni Kanali Benard Mongela amemshukuru Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuwezesha kufanyika kwa zoezi hilo

UONGO FITNA ZAMPONZA MBUNGE MPINA ATAKUWA NJE YA BUNGE KWA VIKAO 15

Image
Spika Dkt. Tulia Ackson na  Katibu wa Bunge  Nenelwa Mwihambi wakibadilishana mawazo wakati taarifa maalum ya bunge kuhusu Mbunge Mpina ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Ally Juma Makoa.   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA     BUNGE LA TANZANIA       TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA    MADARAKA YA BUNGE KUHUSU:-   1.       MAONI YA KAMATI KUHUSU USHAHIDI WA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUTHIBITISHA TUHUMA DHIDI YA WAZIRI WA KILIMO, MHE. HUSSEIN MOHAMED BASHE (MB) KUSEMA           UONGO BUNGENI NA KULIPOTOSHA BUNGE                NA   2.   TUHUMA DHIDI YA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB)          KUDHARAU MAMLAKA YA SPIKA, BUNGE NA             MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE         OFISI YA BUNGE, DODOMA.   JUNI, 2024 TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA   MADARAKA YA BUNGE KUHUSU:-   1.                  MAONI YA KAMATI KUHUSU USHAHIDI WA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUTHIBITI