UCSAF KUENDELEZA JITIHADA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI. MASHIBA
MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa Huduma ya Mawasiliano Vijijini unaendelea ambapo Mfuko huo umesaini mkataba wa kupeleka huduma za Mawasiliano katika kata zaidi ya 1900 na mradi huo umefikia asilimia 90 katika utekelezaji wake. Ameyasema hayo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya UCSAF na kazi ambayo wameifanya ya kuboresha mawasiliano pamoja na kupeleka vifaa vya TEHAMA katika kijiji cha Msomera Mkoani Tanga. Ambapo amesema kuwa jukumu walilokasimiwa na serikali la kuhakikisha wanapeleka mawasiliano vijijini wanalitekeleleza vyema ambapo mpaka sasa kazi kubwa imefanyika ya ujenzi wa minara vijijini na lengo likiwa ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma ya mawasiliano ili kuchochea maendeleo kupitia uchumi wa kidijitali. Tutakapokamilisha ujenzi wa miradi hiyo ya mawasiliano wananchi wapatao milioni 15 watapata huduma za mawasiliano na hii ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo