SAKATA LA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WALIMU (CWT) LAFIKIA PATAMU

Tangazo lililoleta kasheshe likiualifu umma kama mhalifu mwalimu huyu.


Baadhi ya walimu mkoa wa Dodoma ambao ni wanachama wa Chama cha Walimu nchini (CWT), wamemwijia juu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kwa kitendo chake cha kusambaza kwenye mtandao nyaraka ya Serikali inayomhusu katibu Mkuu wa Chama chao, Japheth Maganga cha kukataliwa kuongezwa muda  wa kukitumikia chama hicho.

Walimu hao Juma Ali, Hassan Bakari na Joseph Lupia wakizungumza na mwandishi wa gazeti hili mtandao  walidai wakati Maganga akiazimwa na chama hicho hakuna tangazo kama hilo lililotolewa lakini jambo la kushangangaza imekuwaje sasa nyaraka hiyo iliyotakiwa kuwa ya siri kwakua ni mali ya serikali isambazwe kwenye mitandao.

Kufuatia kitendo hicho wao kwa mitazamo yao wanadai kwamba Katibu Mkuu huyo anapigwa vita na waliowahi kuwa viongozi wa Chama hicho waliotimuli kwa ulaji wa fedha aidha wamemuona anawazibia ulaji huo sasa wanahangaika huku na kule ili kumwondosha.

Wakizungumza na mwandishi wetu wa gazeti mtandao wamesema kufuatia kitendo hicho ambacho si cha kiungwana kwa mtu yeyote sasa wapo tayari kumtete na wanajiandaa kwenda kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wamweleze  jinsi Maganga anavyopigwa vita  na tangu awe katibu mkuu wa Chama hicho faida nyingi zimepatikana pamoja na kupigwa vita.


"Sisi tunafahamu lipo genge ambalo lilikuwa linajinemesha na fedha zetu Magnga kawadhibiti kila kona wanahangaika, wapo radhi kukiua chama kwa ajili ya ubinafsi wao, hatukubali tutamweleza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila kitu", walisema walimu hao kwa uchungu, tunamuomba Rais kwa unyenyekevu kutumia vyombo vyake kwani kunabaadhi ya viongozi wa Serikali wanatumiwa na  aliyekuwa katibu wetu sasa anakesi ya Takukuru kukihujumu chama chetu, Tunaomba aridhie kukutuna na walimu ili abaini yanayoendelea na jinsi anavyozungukwa na kisha wanatisha viongozi wetu huku wakisema ni agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia suluhu Hassan", walisema walimu hao kwa uchungu.

Aidha walibainisha watayafichua hata majumba yao yalipo waliyoyajenga kwa muda mfupi kwa fedha za walimu.

Mbali na hayo pia walimu hao walibainisha kwamba siyo dhambi kuomba kibali cha kuazimwa mara ya tatu ikumbukwe yeye ni katibu wa kuchanguliwa kwanini wasimkubalie  je wanataka atoe notsi ya kuacha kazi ya ualimu ndiyo wafahamu kwamba huku tunamhitaji je angekuwa mkuu wa wilaya wangemlejesha  shuleni  wanadai hapo kuna kitu kinafanyika hakiko sawa, wameomba pia Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi - TUCTA liingilie  kati katika sakata hilo ili wababaishaji wasiruhusiwe kulejea  katika chama hicho.

Walimu hao walibainisha kwamba chama chao kinataka kugeuzwa kama chama cha Kisiasa, baadhi yao wakigombea uongozi wakishindwa au wakitimuliwa kwenye uongozi wanaanzisha  migogoro isiyoisha  na wengine sasa wamediliki kuanzisha vyama vingine vya walimu wakiona hawapati wanachama wanashinikiza migogoro isiyoisha .

Kufuatia sakata hilo walimu hao wameshutumu pia baadhi ya vyombo vya habari kwa kutumika na watu hao, kila mara utasikia waliokataa uteuzi wa Rais wafanya hiki  na kile mara sasa Chama cha walimu kumaliza migogoro baada ya Maganga na Ulaya kuondoshwa, vyombo vinatumika kwa manufaa ya wachache

Kuhusu kusambaza nyaraka za Serikali hivi karibuni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete alisema  sheria inayosimamia nyaraka za Serikali inaelekeza kuwa mawasiliano ya Serikali yafanyike kwa njia ya barua na si vinginevyo.

Kufuatia kuwepo kwa sheria hiyo, Naibu Waziri  Kikwete  aliwaonya watendaji wa Serikali ambao  wanatumia njia ambazo sio rasmi kutuma nyaraka.

“Haitokuwa sawa na ni marufuku ya Serikali kuwasilisha au kutumiiana ‘Documents’ za Serikali kupitia njia ya WhatsApps na njia nyingine zisizo rasmi,” alisema Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Janejelly Ntate James ambaye amehoji uhalali wa  matumizi ya makundi ya WhatsApp kutumiana nyaraka.

Aidha, Naibu Waziri Kikwete alilihakikishia Bunge kuwa  Serikali bado inaendelea kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itaileta ufanisi katika utendaji kazi Serikalini.

Comments

Popular posts from this blog

UNAMKUMBUKA AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIAA.

Je, wajua kwamba Australia ni bara, nchi na kisiwa?

KADA MGEJA AHUDHURIA MAZIKO YA MAMA MZAZI WA MWANDISHI MWANDAMIZI WA HABARI KAHAMA