Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge
Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha
2018/2019 bungeni jijini Dodoma.
Mapema
leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha
Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili
Thelathini na Mbili Elfu.
Kati
ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia
Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa
ajili ya bajeti ya maendeleo.
Pro.
Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba
ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu
Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba.
Sehemu
ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa
mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini
Dodoma .
Mhe.Balozi
Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha
hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Mhe.
Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini
Dodoma
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara.
Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika
viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti
ya Wizara.
Mhe.
Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma
Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa
hotuba ya bajeti ya Wizara
Mhe.
Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara
waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini
Dodoma
Wednesday, May 23, 2018
TFF YATANGAZA MAJINA YA WACHEZAJI 30 WATAKAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA MSIMU HUU
Na Agnes Francis Blogu ya Jamii.
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)limetangaza majina ya wachezaji 30
katika kuelekea mwisho wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
ambao watawania Tuzo za Mchezaji Bora mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa TFF Clifford Ndimbo amesema
utaratibu huo hufanyika kila mwaka baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya
Vodacom kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Vodacom.
Ndimbo
amefafanua wachezaji hao 30 watachujwa na kubaki 10 na baadae watabaki
wachezaji wa tatu wataoinga hatua ya fainali ili kumpata Mchezaji bora
kwa msimu huu.
Amewataja
wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Habibu Kyombo (Mbao),Khamis
Mcha,(RuvuShooting),Yahya Zayd(Azam),Razack Abalora(Azam), Bruce
Kangwa(Azam) Aggrey Morris(Azam),Himid Mao (Azam),Awesu Awesu(Mwadui) na
Adam Salamba(Lipuli).
Wengine
ni Mohammed Rashid(Prisons), Shafiq Batambuze(Singida),Mudathir Yahya
(Singida), Marcel Kaheza(Majimaji),Ditram Nchimbi(Njombe Mji) na Eliud
Ambokile(Mbeya City).
Pia
Shaaban Nditi(Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu(Singida) Ibrahim Ajibu(Yanga),
Gadiel Michael(Yanga),Papy Tshishimbi(Yanga),Kelvin Yondani(Yanga),Obrey
Chirwa(Yanga),Aishi Manula(Simba), Emmanuel Okwi(Simba),John
Bocco(Simba), Jonas Mkude(Simba),
Erasto Nyoni(Simba),Shiza Kichuya(Simba),Asante Kwasi(Simba),Hassan Dilunga(Mtibwa).
"Mchakato
wa kupata mchezaji bora unatarajia kufanyika Juni 23 mwaka huu katika
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ambapo msimu huu kutakuwa
na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet,"amefafanua
Pia
amesema licha ya tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, kutatolewa tuzo
mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine
imeongezwa ikiwa ni katika uboreshaji
"Tuzo
iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili
kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala
ya kuwatenganisha, vile vilee msimu huu imeongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora
Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.Hiyo ni kutokana na kuthamini
nafasi ya waamuzi wasaidizi,"amesema Ndimbo
Kwa
mazingira hayo tuzo zitakazotolewa siku hiyo ambapo wadhamini wakuu ni
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni Bingwa,Mshindi wa Pili,Mshindi
wa Tatu,Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora,Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi,Mwamuzi BoraKipa Bora,Kocha Bora,Goli Bora VPL,Best Eleven,pamoja na Mchezaji wa heshima.
Ndimbo
amesema zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo
ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao
hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.
"Kila
mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya
vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti
kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
"Wachezaji
ambao walishinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu ni nimshambuliaji wa
Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze
(Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba).
"Wengine
ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa
Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John
Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari),
mshambuliaji wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa
Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili),"amesema Ndimbo.
Ambapo
wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na
fedha Sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
WANAWAKE WAJAWAZITO WATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WANAWAKE wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.
“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya na Mkoa.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.
“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”
Jacline Temu, akizunguymza
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon. akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizunguza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kulia kwake ni Mgeni rasmi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon. akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizunguza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kulia kwake ni Mgeni rasmi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon.
KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AWATEMBELEA WANANCHI JAMII YA WAHADZABE NA WATATOGA HUKO ESHKESH WILAYANI MBULU MKOA WA MANYARA
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati
alipotembelea Kata ya Eshkesh kijiji cha Dumanga Yaeda Chini wilayani
Mbulu mkoa wa Manyara wakati alipozitembelea jamii hizo ili kuzungumza
nao kuhusu maisha yao pamoja na uhifazi wa tamaduni na mila zao ambao
unaweza kuwa Kivutio cha Utalii pia lakini pia kujua mahitaji yao ya
muhimu katika maisha ya jamii hizo.(PICHA NA JOHN BUKUKU
FULLSHANGWE-MBULU)
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati
alipotembelea Kata ya Eshkesh kijiji cha Dumanga kutoka kulia ni Gesso
Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu., Kaimu Mkurugenzi wa
Utamaduzi Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Beleko na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.
Wananchi wa Eshkesh Jamii ya Watatoga wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza katika mkutano huo.
Gesso Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu akizungumza katika mkutano huo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akimtunza mmoja wa vijana aliyekuwa akicheza ngoma ya kisukuma katika
mkutano huo.
Mmoja wa vijana wapiga ngoma akipiga ngoma kwa mbwembwe wakati kikundi cha ngoma ya kisukuma kikitumbuiza.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw.
Hudson Kamoga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan katikati na
Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni Bi.
Liliano Beleko wa pili kutoka kushoto wakicheza ngoma na akina mama wa
jamiii ya Wahadzabe katika kijiji cha Dumanga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimpa
pole mama aliyejifungua na kupoteza manaye alifariki baada ya kuzaliw.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akizungumza na Mmoja wa akina mama wa kihazabe nyumbani kwake Jamii ya
Wahadzabe wananawake ndiyo wanaojenga nyumba kazi ya wanaume ni kuwinda
wanyama na kurina asali pamoja na kutafuta mizizi kwa ajili ya chakula.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akitoka katika moja ya nyumba ya familia ya kihdzabe.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akifurahia jambo baada ya kuvaliswa zawadi ya mkanda uliotengenezwa kwa
Shanga na Bi.Chrstina Paulo mama wa jamii ya Kihadzabe.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi
akivishwa mkanda uliotengenezwa kwa Shanga na Bi.Chrstina Paulo mama wa
jamii ya Kihadzabe.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakikimbia na akina mama wa
Kihadzabe huku wakiimba kuelekea eneo la makazi yao mara baada ya
kupokelewa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakicheza na akina mama wa
Kihadzabe huku wakiimba kuelekea eneo la makazi yao mara baada ya
kupokelewa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakipokelewa na wananchi wa
Dumanga wa jamii ya Kitatoga mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakipokelewa na ngoma ya
akina mama wa Kihadzabe
Vijana wa Kitatoga wakiimba katika mapokezi hayo.
Comments
Post a Comment