Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima . Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo . Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vit