Leo ni Miaka Mitano ya Kumbukumbu ya Kifo cha Amina Chifupa Mpakanjia Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya. Amina leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena katika Redio ya Clouds FM. Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania wataendelea kumuenzi na atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa dawa ya kulevya. Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini. Pumzika kwa Amani Amina Chifupa! Chini ni picha za baadhi ya matukio mbalimbali ambayo Amina chifupa aliweza kushikiriki wakati wa Uhai wake. Picha Hizi zilipigwa enzi hizo Amina Chifupa alipenda mich
Kangaroo hupatikana Australia pekee Miamba Bahari ya Australia ni mikubwa kuliko yote Duniani na kivutio kwa watalii Ramani ya Australia Robo tatu ya Waustralia wanaishi katika majiji makubwa na maeneo ya pwani. Fukwe pia ni sehemu za utambulisho wa Australia SAYARI tuishimo yaani dunia ina mabara saba, ambayo tukianzia kwa mtiririko wa bara kubwa hadi dogo ni Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Ulaya, Antarctica na Australia Mbali ya mabara hayo ambayo Antartica ni pekee lisilokaliwa na watu kutokana na kufunikwa na barafu kwa asilimia 89, dunia ina nchi huru kati ya 180 na 195 huku ikiwa na mamia kwa maelfu ya visiwa. Katika makundi hayo matatu, Australia ni pekee duniani iliyobeba sifa zote tatu yaani bara, nchi na kisiwa, kwani nyingi zimeishia kuwa na sifa moja au mbili yaani nchi na au kisiwa. Australia ni bara dogo kuliko yote duniani, lakini pia kisiwa kikubwa kuliko vyote katika sayari hii. Mbali ya sifa hizo mbili pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja (mwenye kibaghalashia), ameungana na familia ya mwandishi mwandamizi wa habari, Mohab Dominick, katika maziko ya mama yake mzazi, Tekra Limi, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91. Maziko hayo yalifanyika katika makaburi ya Kanisa Katoliki Mbulu, katika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga. Viongozi mbalimbali wa chama na serikali walihudhuria tukio hilo, wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu na pole kwa familia iliyoachwa. Akizungumza katika maziko hayo, Mgeja alitoa neno la faraja kwa familia ya Mohab Dominick, akiwatia moyo kuwa Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.Alisema kuwa ingawa ni kipindi kigumu, wanapaswa kuwa na imani na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, \ameungana na familia ya mwandishi mwandamizi wa habari, Mohab Dominick, k
Comments
Post a Comment