Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu
Wizara ya afya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa wa Malaria kinakusudia kutoa vyandarua laki moja na 95 elfu kwa mama wajawazito na watoto waliochini ya miaka mitano nchi nzima .
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar juu ya uzinduzi wa Kampeni ya kubwa ya matumizi ya vyandarua ambayo inatarajiwa kufanyika April nne mwaka huu visiwani Zanzibar Meneja wa utaribu wa kazi za kumaliza Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ali amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimokatika mchakato wa kumaliza Malaria ambapo kwa sasa ni zaidi ya miaka kumi Zanzibar imekuwa ikipambana na ugonjwa huo .
Amesema Zanzibar kila kipindi kinachomaliza mvua za masika kumekuwa na kiwango kikubwa ugonjwa Malaria lakini jitihada mbali mbali zinachukuliwa ikiwemo kupiga dawa majumbani, kuhakikisha dawa zinapatikana katika vituo vya afya, na kuwepo kwa vipimo cha kuchunguzia ugonjwa huo na matumizi ya vyandarua vilivyopigwa dawa.
Amesema vyandarua ndio kinga tahabiti ya kujikinga na Malaria ambapo kwa Zanzibar Asilimia 77 ya Wananchi wanatumia vyandarua kiwango ambacho bado hakijaridhisha kufikia vigenzo vya wizara ya afya zanizbar ya Asilimia 100 na shirika la afya ulimwenguni WHO Asilimia 85.
Hata hivyo Meneja Abdallah amesema kwa sasa licha ya Zanzibar kupunguza maambuzi ya wagonjwa wa Malaria lakini amekiri ugonjwa huo bado upo chini ya Asilimia moja na ambapo vigezo vinavyotumika kuhakikisha Wananchi wanaobainika kuwa na vimelea anafuatiliwa katika familia yake ili kuhakikisha anakuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.
Aidha amesema bado kuna maeneo ambayo yanatoka wagonjwa wengi wanaobainika kuwa na vimelea vya Malaria ikiwemo Wilaya ya Maghariba A na B , Wilaya ya kati na Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba na kwa wale Wananchi ambao wanatoka Tanzania bara katika mikoa ya Mwanza na Geita.
Kwa upande wake Waziri Nyoni Meneja Miradi wa VectorWorks amesema watakuwa na kazi ya kuhamasisha Jamii kuhakikisha vyandarua wanavyopatiwa wanavitumia ipasavyo ili kujikinga na ugonjwa na Malaria.
Kampeini ya kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP .
Meneja wa kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar Abdallah Suleiman Ally akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria.
Meneja Miradi kutoka VectorWorks akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar wakati akitangaza kuanza kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti
MAANDALIZI YA MFUMO WA PAMOJA WA KIELEKTRONIKI WA UONDOSHAJI SHEHENA YAANZA
Serikali
imeanza maadalizi ya kutengeneza Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa
Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na
Mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za
Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau
mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni
kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.
“Uwepo
wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia
mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja
na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha
zaidi”, alisema Kichere.
Kichere
alieleza kuwa, uwepo wa wakuu hao na wadau wa sekta binafsi katika
mkutano huo ni kiashiria cha kuunga mkono adhma ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya
mipaka ya Tanzania.
Kamishna
huyo Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliongeza kuwa, Serikali
imelenga kuwawezesha wadau wote wanaohusika na biashara za kimataifa na
usafirishaji wa mizigo kutumia Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa
Uondoshaji Shehena kwa lengo la kuwezesha uwasilishaji wa nyaraka mahali
pamoja ili wadau wote waweze kushughulikia nyaraka hizo kwa wakati.
Naye
Mratibu wa Mfumo wa Uondoshaji Shehena kutoka TRA Felix Tinka amezitaja
faida za mfumo huo kuwa ni pamoja na kurahisisha na kuwezesha
biashara, kuongeza ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali na kuongeza
uhiari wa ulipaji ushuru na tozo mbalimbali kwa waingizaji na
waondoshaji wa mizigo.
“Mfumo
huu una faida nyingi, mbali na hizo nilizozitaja awali, pia kuna
kuimarisha usalama, kuimarisha uadilifu na uwazi katika utendaji kazi,
kupunguza biashara haramu, kupunguza gharama, kupunguza muda wa
uondoshaji mizigo katika vituo vya forodha pamoja na kurahisisha
ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati”, Alisema Tinka.
Utekelezaji
wa Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini,
Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani umegawanyika katika maeneo
makuu matano ambayo ni eneo la usimamizi wa mapato, uwezeshaji wa
usafiri na uchukuzi, utekelezaji wa sera na biashara, pamoja na
usimamizi wa afya na usalama wa umma, usalama wa uchumi pamoja na
ugawaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akitoa mchango wake wakati wa mkutano huo. |
Katibu Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Abel Urono akitoa mchango wake katika mkutno huo. |
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere (kulia) akibadilishana mawazo na Nibu Kamishna wa TRA, Zanzibar Mcha Hassan baada ya kuhudhuria mkutano huo. |
Mshauri wa Tehama, Abdulrahman Mbamba akitoa mada kwa washiriki wa Mkutano huo. |
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mijadala kwenye mkutano huo. |
DK. KIGWANGALLA APOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA WANAOTAKA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UTALII
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya
pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia
Leasing kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati
kampuni hiyo ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Na Hamza Temba - WMU-Dodoma
...........................................................................
Kufuatia
jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kutafuta wawekezaji wa
Kimataifa kwa ajili ya kuwekeza katika sekta utalii hapa nchini, Kampuni
ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini China
imejitokeza kwa lengo la kuwekeza katika utoaji wa huduma za kitalii
zenye ladha na mandhari ya Kichina.
Mwenyekiti
wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Tony, amesema
kampuni hiyo imepanga kujenga hoteli za kitalii za kichina katika mji wa
Karatu jijini Arusha na Serengeti mkoani Mara.
Akizungumza
na Waziri wa Maliasil na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ofisini kwake
mjini hapa jana kwa ajili ya kutambulisha mradi huo, Tony alisema mradi
huo ni mahsusi kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii wa China
wanaotembelea Tanzania.
Alisema
kupitia mradi huo jumla ya magari 500 ya safari za utalii yatanunuliwa
(Safari Cars) kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii hao wakati wa
kutembelea maeneo ya vivutio hapa nchini.
Pamoja
na magari hayo alisema kampuni hiyo pia imepanga kuanzisha safari za
moja kwa moja za ndege kutoka China hadi Tanzania ili kupunguza muda wa
usafiri na gharama.
"Kupitia
mradi huu, tunategemea kuhudumia watalii 200,000 kwa mwaka kutoka
nchini China na kutengeneza ajira zaidi ya 200 kwa Watanzania" alisema
Tony.
Alisema
kwa sasa ni watalii 35,000 tu kutoka China wanaotembelea Tanzania kwa
mwaka, na kwamba kupitia mradi huo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.
Naye
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema mradi huo
umekuja wakati muafaka wakati huu Serikali kupitia Wizara yake
imeshaweka mikakati mahususi ya kupanua wigo wa soko la utalii nchini
China.
Alisema
miongoni mwa mikakati hiyo inayolenga kuvutia watalii zaidi ya 200,000
kwa mwaka katika kipindi cha muda mfupi wa miaka mitatu, ni
kuwakaribisha wachina wenyewe kuja kuwekeza kwenye mahoteli na huduma
zenye ladha na mandhari ya kikwao. Mataifa mengine ni Israel, Urusi na
Oman.
Alisema kwa sasa ni idadi ndogo tu ya watalii wa China wanaotembelea Tanzania ukilinganisha na ukubwa wa soko la nchi hiyo.
Aliahidi
kuwapa ushirikiano wawekezaji hao ikiwa ni pamoja na kuwapa maeneo kwa
ajili ujenzi wa hoteli hizo za kitalii ndani ya maeneo ya hifadhi ili
kuwezesha ongezeko la watalii kutoka nchini humo.
"Kwa
yale maeneo mtakayohitaji ambayo yapo nje na maeneo yetu ya hifadhi
tunayoyasimamia, tutawasiliana na mamlaka husika ili muweze kuapatiwa
maeneo ya kuanzisha uwekezaji huo muhimu kwa taifa" alisema Dk.
Kigwangalla.
Aliwataka
pia wawekezaji hao kupitia taratibu zote za kuwekeza hapa nchini ikiwa
ni pamoja na kujisajili katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Kusajili kampuni ya utalii hapa nchini na kuwasilisha andiko la mradi na
namna ya utekelezaji wake.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing
kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Wawekezaji
wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini
China wakiwa kwenye mazungumzo na Waziri Kigwangalla ofisini kwake mjini
Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi flash yenye
picha za wanyamapori wa Tanzania Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya
Tibet Dexin Financia Leasing, aliyefahamika kwa jina moja la Tony kutoka
nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza hapa nchini katika ujenzi wa
mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Waziri Kigwangalla akiendelea na mazungumzo na wakezaji hao.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wawekezaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing
kutoka nchini China ofisini kwake mjini Dodoma jana wakati kampuni hiyo
ilipowasilisha mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
Mazungumzo yakiwa yanaendelea.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na wawekezaji
wa Kampuni ya Kimataifa ya Tibet Dexin Financia Leasing kutoka nchini
China ofisini kwake mjini Dodoma jana baada ya kampuni hiyo kuwasilisha
mpango wake wa kuwekeza apa nchini katika ujenzi wa mahoteli na huduma za utalii zenye ladha na mandhari ya kichina.
BancABC YATEKELEZA SERA YA FEDHA YA BoT
Mkurugenzi
mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali
katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo ya
mikopo mbali mbali kwa wateja wao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha
Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha
wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Malai katikati
wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.
BENKI
ya BancABC imesema imetekeleza Sera ya fedha ya Benki Kuu ya
Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja wake wapya
kuwezesha kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha
amesema benki hiyo ni sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa katika soko
la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika
masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na
uwezo wa kukuza mitaji.
Hivyo
Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya
masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na ya nyumba na
kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa
ukwasi.
"Hivyo
kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali
kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa
kupunguza masharti kama vile kiwango cha chini cha fedha kwa
mabenki,"amesema Botha.
Ameongezea viwango vya punguzo,hati fungani za hazina na kukopesha
mabenki
kwa viwango vya chini na hiyo imewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na
kampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha
uchumi. "Na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi
kuhusu punguzo hili."
Aidha
Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo amesema kuwa benki
hiyo inahudumia wateja zaidi ya 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti
za kibenki
Mwasomengo
amesema fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja kupata mikopo ya
Nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa Daraja la
kati na chini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara
wa BancABC Joyce Mlai amemalizia kwa kusema katika kujenga nyumba
wanaungana na Serikali kuwapa fursa ya kuwapatia mikopo ya Nyumba
wafanyakazi wa aina zote sekta binafsi,serikalini pmoja na wafanya
biashara.
Comments
Post a Comment