Posts

Showing posts from January, 2018

CHUO CHA KODI KUWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA FORODHA ZANZIBAR

Image
Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar (ZFB) Omar Hussein Mussa wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano katika kuwajengea uwezo wanachama wa ZFB. Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar Omar Hussein Mussa wakizungumza na wajumbe wa Kamati ya Makubaliano kutoka Chuo cha Kodi (Kulia) na Zanzibar (kushoto) kabla ya kusaini hati za makubaliano katika chumba cha mikutano ITA. Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Forodha Zanzibar (ZFB) Omar Hussein Mussa (wa pili Kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Tanzania (TAFFA) Stephen Ngatunga (wa kwanza kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ushirikiano mara baada ya kusaini makubaliano ya kuwajengea uwezo mawakala wa Forodha Zanzibar. (PICHA ZOTE NA OLIVER NJUNWA). ……………………

ADAM MALIMA AANZA KUWASHUGHULIKIA WALIOHUJUMU KIWANDA CHA MAZIWA CHA UTEGI

Image
UFAFANUZI: Mkuu wa Mkoa wa Mara (RC), Adam Malima (wa pili kushoto) akimsikiliza mmoja wa watu wanaodaiwa kuunda Kampuni ya UDAFCO akitoa maelezo kwenye kikao cha RC Malima huku Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (kushoto) na viongozi wengine wakisikiliza mgogoro wa shamba la mifugo na kiwanda cha maziwa cha Utegi. Picha Na Peter Fabian.   Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (wapili kulia) aliyekaa akipitia nyaraka za mfanyabiashara ambaye ni mwekezaji wa shamba la mifugo na kiwanda cha maziwa cha Utegi kwenye kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya juzi ikiwa ni agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilolitoa hivi karibuni wengine Mwekezaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya UDAFCO, Otieno Igogo (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha (wapili kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo (wa kwanza kushoto).   Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akihutubia wananchi wa vijiji sita kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mji wa Utegi kusikili

NG'OMBE ZAIDI YA 341,098 WAPIGWA CHAPA SIMANJIRO

Image
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (wapili kulia) baada ya kupewa zawadi ya nguo ya jadi na wafugaji wa kata ya Naisinyai kwenye ziara yake Wilayani Simanjiro, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Jackson Leskar Sipitieck na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Arnold Msuya.  Ng'ombe 341,098 wamepigwa chapa Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ili kutekeleza agizo la Serikali la upigaji chapa mifugo kwa ajili ya utambuzi na kuepuka migogoro ya mara kwa mara.  Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary, aliyasema hayo juzi wakati akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti.  Omary alisema lengo la wilaya hiyo ni kupiga chapa ng'ombe 437,925 hivyo wamefikia asilimia 79 hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana.  Alisema zoezi hilo lilitarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka jana ila baada ya serikali kuongeza muda hadi Januari 31 mwaka huu, watakuwa wa

NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Image
Binti mwenye umri chini yaa miaka 18 akiwa amembeba motto wake mdogo baada ya kukatishwa ndoto zake za kupata masomo na kijana. baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.  baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.  Meneja wa World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja Kulangwa akiwasilisha mada juu ya madhumuni ya semina hiyo kwa wananchi waliohudhuria kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida. Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alipokuwa akizindua mpango wa mapambano dhidi ya ndoa za utotoni kwenye ukumbi wa Kanis Katoliki,mjini Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly). Na,Jumbe Ismailly SINGIDA  TATIZO la ndoa za utotoni katika Tanzania na nchi za Afrika Mashariki limeonekana ni tat