NG'OMBE ZAIDI YA 341,098 WAPIGWA CHAPA SIMANJIRO
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (wapili kulia) baada ya kupewa
zawadi ya nguo ya jadi na wafugaji wa kata ya Naisinyai kwenye ziara
yake Wilayani Simanjiro, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo mhandisi Zephania
Chaula na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
Jackson Leskar Sipitieck na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Arnold
Msuya.
Ng'ombe
341,098 wamepigwa chapa Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ili
kutekeleza agizo la Serikali la upigaji chapa mifugo kwa ajili ya
utambuzi na kuepuka migogoro ya mara kwa mara.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary, aliyasema hayo juzi wakati
akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti. Omary
alisema lengo la wilaya hiyo ni kupiga chapa ng'ombe 437,925 hivyo
wamefikia asilimia 79 hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana.
Alisema
zoezi hilo lilitarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka jana ila baada
ya serikali kuongeza muda hadi Januari 31 mwaka huu, watakuwa
wamefanikiwa kukamilisha. Alisema
wilaya hiyo ina mabwawa mawili ya Nyumba ya Mungu na Kidapash, ambayo
shughuli za uvuvi zinafanyika na jitihada za kudhibiti uvuvi haramu
zimefanyika.
Kwenye
sekta ya kilimo, umwagiliaji na ushirika alisema kuna ekari 346,000
zinazofaa kwa kilimo ambapo takribani ekari 144,00 hutumika kwa kilimo
cha mazao ya chakula na biashara. "Mahitaji
ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wote ni tani 42,000 za nafaka na hali
ya chakula ni ya kuridhisha kwenye maeneo mengi kwani wananchi wanatumia
chakula kilichovunwa msimu wa Kilimo wa 2016/2017.
Alisema
kwa upande wa mradi wa maji kutoka mto Ruvu hadi mji mdogo wa
Orkesumet, serikali itautekeleza kupitia sh40 bilioni, za fedha za ndani
na ufadhili wa benki ya maendeleo ya watu wa uarabuni. Mkuu
wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti aliagiza kila wilaya ya mkoa huo
kuhakikisha inakuwa na viwanda 15 ili kutekeleza agizo la serikali la
kila mkoa uwe na viwanda 100.
Mnyeti
alisema wilaya ya Simanjiro iwe na viwanda 15 na nyingine zitekeleze
hilo ili kuhakikisha uzalishaji wa ajira unafanyika na kufikia lengo la
kuwa na uchumi wa kati.
WAKULIMA SKIMU YA UMWAGILIAJI MPUNGA NYAMAGOGO MANYONI WALALAMIKIA HALMASHAURI KUTELEKEZA KATAPILA
Na Jumbe Ismailly-Manyoni
WAKULIMA
wa skimu ya umwagiliaji mpunga ya Nyamagogo,iliyopo katika Kijiji cha
Chikuyu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wameiomba serikali kuangalia
uwezekano wa kuitengeneza katapila lililokuwa likisaidia kusafisha
mifereji ya kuoitisha maji kwenye mashamba hayo ili waweze kuongeza
uzalishaji wa zao hilo ambao kwa sasa umepungua.
Mwenyekiti
wa skimu hiyo ya umwagiliaji Nyamagogo,Abdallah Rajabu Maganga alisema
katapila hilo ambalo limetelekezwa tangu mwaka 2012 kutokana na
kukosekana kwa vipuli vinavyohitajika kulifufua kwa sababu kifaa hicho
ni aina ya kizamani na hivyo matengenezo yake siyo rahisi na badala yake
lingefaa kuuzwa kwa njia yam nada.
“Tatizo
wanavyosema sema ni greda la kizamani unaona bwana spea zake
hazipatikani sasa tunajiuliza wanaproses kwamba wanataka kuliuza unaona
bwana sasa huyo unayemuuzia atalifanyia nini kama kweli ni greda la
zamani ambapo hakauna spea”alifafanua Maganga.
Alifafanua
mwenyekiti huyo wa (WAUWA) kwamba ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo
na kwa sababu sasa hivi dunia ni ya utandawazi spea zinapatikana sehemu
yeyote pale hata kama Marekani wanaweza kwenda au kuagiza ili liweze
kutengenezwa kwa manufaa ya wakulima hao wa skimu ya umwagiliaji.
Mwenyekiti
huyo hata hivyo aliyataja baadhi ya athari wanazopata wakulima hao kuwa
ni pamoja na kujaa kwa maji ambayo hupeleka na mchanga na kusababisha
mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,lakini endapo wangelipata greda
hilo lingeweza kuwasaidia kutoa michanga na maji kufuata mkondo wake
unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea bure huku
kipato chao kikipotea.
Naye
diwani wa kata ya Chikuyu,Benjameni Kamoga alisema kuwa kwa taarifa za
awali kutoka Halmashauri zilisema kinachosumbua katapila hilo ni
kukosekana kwa cheni ambayo inahitaji nguvu katika matengenezo ili
wakulima waweze kunufaika na kuwepo kwa miundombinu hiyo ya kilimo.
“Kwa
mfano kuna mikato ambayo imesababishwa na maji kujaa pamoja na ujenzi wa
nguzo za umeme,Tanesco walikuja wakatuzibiazibia lakini hawakujua
ukubwa, kwa maana hiyo kama lingekuwa zima hili lingetufanyiakazi
nzuri”.alibainisha diwani Kamoga.
baadhi
ya Skimu za umwagiliaji mashamba ya mpunga Nyamagogo,wilayani
Manyoni,Mkoani Singida yaliyoathirika kutokana na kujaa kwa maji ambayo
hupeleka na mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata
mikato,kwa sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na
maji kufuata mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji
mengi yanapotea bure huku kipato chao kikishuka.
baadhi
ya mitaro iliyojaa mchanga pamoja na takataka na hivyo kusababisha maji
kukosa mwelekeo na hivyo kusambaa ovyo kwenye maeneo mengine.
Katapila
lililokuwa likiwasaidia wakulima wa skimu ya umwagiliaji mpanga
Nyamagogo,wilayani Manyoni,Mkoani Singida kutojaa kwa maji ambayo
hupeleka mchanga na kusababisha mto kuwa juu na kuanza kukata mikato,kwa
sababu ya kukosekana kwa katapila litakalotoa michanga na maji kufuata
mkondo wake unaokubalika badala ya hivi sasa ambapo maji mengi yanapotea
bure huku kipato chao kikishuka.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
KAMISHNA JENERALI MAGEREZA, DK. JUMA MALEWA ATETA NA MAHABUSU GEREZA KEKO MAADHIMISHO WIKI YA SHERIA NCHINI
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la
Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua
gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika
sekta ya Sheria hapa nchini.Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa
Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah
alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni
sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo. Mkuu
wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi
Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(hawapo pichani).Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza
hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu
ambaye ni raia wa kigeni mara baada ya kuongea na Mahabusu wa Gereza
Keko.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akikagua jiko la gesi
katika Gereza la Mahabusu Keko. Jeshi la Magereza tayari limeanza
kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuachana na matumizi ya kuni kwa
kutumia nishati ya gesi katika baadhi ya magereza nchini hivyo kutunza
mazingira.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza
Keko ambapo chumba hicho kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli
mbalimbali kwa kutumia njia ya TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia
gharama Jeshi la Magereza katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na
kuwarejesha magerezani.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika
Chumba Maalum ambacho kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa
kutumia njia ya TEHAMA(wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Noel James(wa kwanza
kulia) ni Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi
Abdallah (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Comments
Post a Comment