NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Binti mwenye umri chini yaa miaka 18 akiwa amembeba motto wake mdogo baada ya kukatishwa ndoto zake za kupata masomo na kijana.
baadhi
ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi
ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini
Singida.
baadhi
ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa semina ya mapambano dhidi
ya ndoa za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki,mjini
Singida.
Meneja
wa World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya kati,Faraja Kulangwa
akiwasilisha mada juu ya madhumuni ya semina hiyo kwa wananchi
waliohudhuria kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini
Singida.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo alipokuwa akizindua mpango wa
mapambano dhidi ya ndoa za utotoni kwenye ukumbi wa Kanis Katoliki,mjini
Singida.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Na,Jumbe Ismailly SINGIDA
TATIZO
la ndoa za utotoni katika Tanzania na nchi za Afrika Mashariki
limeonekana ni tatizo kubwa sana katika maeneo hayo ambapo kitakwimu
inaonyesha kuwa kati ya mikoa kumi bora Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa
kuwa na asilimia 59 na Mkoa wa Singida umeshika nafasi ya nane kwa kuwa
na asilimia 42.
Meneja
wa Shirika la kidini lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania
(WVT) Kanda ya kati,Faraja kulanga aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa
mpango wa kutokomeza mimba za utotoni uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Kanisa Katoliki,mjini Singida.
Alifafanua
kwamba kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tanzania Demokratic Health
Survey ya mwaka 2010 inaonyesha kitakwimu kwamba tatizo la ndoa za
utotoni,Mkoa unaoongoza ni Mkoa wa Shinyanga wenye asilimia 59 huku Mkoa
wa Singida ukiwa na assilimia 42 na hivyo kushika nafasi ya nane katika
mikoa hiyo kumi bora.
“Kwa
maana kwamba ule utafiti huwa unakwenda kuuliza kila nyumba na wakiuliza
katika kila nyumba mama alipata ujauzito katika umri gani,wale
waliopata mimba katika umri chini ya miaka 18 ilikuwa ni asilimia
59.”alifafanua Kulanga.
Kwa
mujibu wa Meneja huyo katika asilimia 42 ya familia zilizoulizwa kina
mama kwamba alipata ujauzito akiwa na umri chini ya miaka 18,asilimia 42
wakaonekana ilikuwepo na kwamba shirika hilo lilifanya utafiti katika
Kanda saba kwenye maeneo wanayofanya kazi.
Aidha
Meneja huyo aliweka bayana kwamba kanda hiyo ina jumla ya kanda saba
ambazo ni pamoja na Kanda ya Pwani ambayo ndiyo inayoongoza ikifuatiwa
na kanda ya kati ambayo ni pamoja na Mkoa wa Singida ambapo kitakwimu
inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la ndoa za utotoni.
Kwa
upande wake Afisa wa dawati la jinsia na Watoto kutoka jeshi la polisi
wilaya ya Singida,Amina Fakih Abdallah alibainisha kuwa kinachochangia
kwa namna moja au nyingine kuwepo kwa ongezeko la mimba za utotoni ni
ukinzani wa sheria zinazosimamia mimba za utotoni.
Hata
hivyo afisa huyo wa dawati la jinsia na watoto alisisitiza pia kwamba
katika sheria zinazosimamia ndoa hizo za utotoni,hakuna sheria
iliyosimama na inayolinda mimba za utotoni kutokana na moja ya sheria
hizo kuruhusu mtoto aolewe akiwa na umri wa miaka 14 huku sheria ya
jinai inakataza motto mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.
“Sasa
kama inalinda mimba za utotoni kuna sheria inaruhusu mtoto wa kike
aolewe akiwa na umri wa miaka 14,sasa hii sheria inaporuhusu mtoto
aolewe akiwa na umri wa miaka 14,we huku kwenye sheria ya jinai unasema
kwamba huyu mtoto aliye chini ya miaka 18 haruhusiwi kuolewa”alifafanua.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Singida,Eliasi Tarimo akizindua Mpango wa mapambano
dhidi ya kutokomeza ndoa za utotoni za mradi wa Mtinko ADP uliopo wilaya
ya Singida alisisitiza pia juu ya kuondoa mapungufu yaliyopo katika
sheria zinazosimamia mimba za utotoni ili ziweze kufanana badala ya
kuendelea kukinzani.
Kwa
mujibu wa Tarimo ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
katika wilaya hiyo sheria zote hizo hazina budi kutamka bayana kwamba
umri wa motto usizidi miaka 18,ikiwemo sheria ya ndoa,sheria ya motto
mwenyewe na kipengere kinachotamka kuwa motto anaweza kuolewa kwa kibali
cha wazazi.
Comments
Post a Comment